Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi amefanya Uteuzi wa Nyadhifa Mbali Mbali katika Wizara na Taasisi za Umma   kama ifuatavyo:-

 

Capt. Khatib Khamis Mwadin ameteuliwa kuwa Naibu Mkuu wa Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo (KMKM).

 

Bwana Mudrik Fadhil Abass ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Maji katika Wizara ya Maji, Nishati na Madini.

 

Bwana Nassor Shaaban Ameir ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Uvuvi Zanzibar (ZAFICO).

 

Uteuzi huo unaanzia leo tarehe 8 Oktoba, 2021.

Download File: