RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi amekutana na Rais wa Shirikisho la Jamhuri ya Somalia Mhe. Dk. Hassan Sheikh Mohamud, Ikulu ndogo ya Migombani, Zanzibar.

Katika mazungumzo yao, Rais Dk. Mohamud amempa pole Rais Dk. Mwinyi kutokana na kifo cha baba yake mzazi, Marehemu Mzee Ali Hassan Mwinyi, (Rais Mstaafu wa Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania) aliefariki dunia tarehe 29 Februari mwaka huu.

Rais Dk. Mohamud alikua ziarani nchini kwa siku mbili kufuatia mwaliko rasmi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan hivi karibuni.Pia, Rais Dk. Dk. Mohamud alihudhuria maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano wa Tanzania.