Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi amewanasihi Waumini wa Dini ya Kiislamu Kutenda Mambo Mema ili kutajwa kwa Wema ndani ya Jamii pale wanapotangulia mbele ya Haki. Alhaji Dkt, Mwinyi ameyasema hayo leo tarehe 16 Januari 2026 alipojumuika na Waumini wa Dini ya Kiislamu katika Ibada ya Sala ya Ijumaa iliyosaliwa Msikiti wa Bamita Chumbuni ,Mkoa wa Mjini Magharibi
Kwa Mnasaba huo ,Alhaji Dkt, Mwiyi amesema Serikali imekuwa Ikiendeleza Miradi mbalimbali ya Maendeleo nchini kote ikiwa ni juhudi za Serikali kuhakikisha inatimiza Matarajio Makubwa walionayo Wananchi. Naye Katibu Mtendaji wa Afisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar , Sheikh Khalid Ali Mfaume ametoa Wito kwa Waumini wa dini ya Kiislamu kutafuta Elimu zaidi ili kujijengea Heshima ndani ya Jamii.
Naye, Khatibu wa Msikiti huo Sheikh Suleiman Nassor amewasihi Waumini wa Dini ya Kiislamu kuzidisha Upendo na Umoja baina yao pamoja na kutafuta Elimu kwani ni muhimu kwa Maisha ya kila siku ya Mwanadamu pamoja na Kuwahimiza kuzidisha Ibada katika Miezi Mitukufu katika Dini ya Kiislamu. Aliyekuwa Rais wa Awamu ya Pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Ali Hassan Mwinyi aliweka Jiwe la Msingi na Kusali katika Msikiti huo wa BAMITA Mwaka 1981.
Alhaji Dkt, Mwinyi amnaendeleza Utaratibu wake wa kujumuika na Waumini wa Dini ya Kiislamu katika Sala ya Ijumaa katika Misikiti mbalimbali Mjini na Vijijini.