Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi amewaachia huru Wanafunzi 17 wa chuo cha Mafunzo katika Maadhimisho wa miaka 62 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar Tarehe 12 Januari, 2026.

Kwa mujibu wa Uwezo aliopewa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,chini ya kifungu cha 59 cha katiba ya Zanzibar ya Mwaka 1984 cha kutoa msamaha kwa mtu aliyehukumiwa kwa kosa lolote,Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ametumia mamlaka hayo ya Kikatiba kutoa Msamaha katika kuadhimisha Miaka Sitini na Mbili (62) ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Katika Msamaha huo,jumla ya Wanafunzi Kumi na Saba (17) waliokuwa wakitumikia adhabu zao katika Chuo cha Mafunzo wameachiwa huru, ambapo kati yao Wanafunzi Kumi na Moja (11) ni wa Unguja na Wanafunzi Sita ni wa Pemba.

Hatua hii ni utaratibu wa kawaida kwa  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kutoa msamaha kwa baadhi ya Wanafunzi wa Chuo cha Mafunzo katika maadhimisho ya kitaifa kama haya.