Taarifa kwa Vyombo vya Habari.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi anatarajia kufanya ziara ya kikazi ya siku tano kisiwani Pemba kuanzia kesho Jumatatu tarehe 30 Agosti mpaka tarehe 3 Septemba 2021.

Katika ziara hiyo, Mhe. Rais atatembelea na kukagua miradi mbalimbali ya kimaendeleo kwenye Mikoa ya Kaskazini Pemba na Kusini Pemba pamoja na wilaya zake.

Hii ni ziara rasmi ya kikazi ya Mhe. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi kuifanya kisiwani Pemba ambapo pia atatumia fursa hiyo kuzungumza na wananchi kupitia makundi mbalimbali kwa nyakati tofuati.

Download File: