Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Mwinyi ameeleza kutoridhishwa kwake na utendaji kazi wa mamlaka za Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa yakiwemo Mabaraza ya Miji, Halmashauri na Manispaa za Zanzibar.


Mhe. Rais ameyasema hayo alipokutana na viongozi wote wa Serikali za Mitaa kutoka mikoa yote ya Zanzibar wakiwemo Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya zote za Unguja na Pemba, Ikulu Zanzibar.Katika kikao hicho, Mhe. Rais amewataka Wakuu wa Mikoa na Wilaya kuhakikisha suala la Ulinzi, Amani na Usalama katika maeneo yao linasimamiwa na kupewa kipaumbele namba moja.


Aidha, Mhe. Rais amezitaka mamalaka za Manispaa na Mabaraza ya Miji yanasimamia ukusanyaji wa mapato na matumizi yatakayoleta tija katika kuwaletea wananchi maendeleo pamoja na kuhakikisha miji inakuwa safi na yenye kuvutia.