Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amewateua wafuatao kuwa Wakuu wa Mikoa na Manaibu Makatibu Wakuu katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kama wafuatao:-

1. Mheshimiwa  Moh'd Ali Abdallah ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharib.  Kabla ya Uteuzi Mhe. Moh'd  alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Mjini Unguja.

2. Mhe. Cassian Galos Nyimbo ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja. Kabla ya Uteuzi huo Mhe. Cassian  alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Magharibi “A” Unguja

3. Mhe. Mgeni Khatib Yahya ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba .Kabla ya Uteuzi Mhe. Mgeni alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake Pemba.