State House Blog

Rais wa Zanzibar Mhe Hussein Mwinyi amewatembelea Wazee mbalimbali kwa ajili ya kuwajulia hali zao.

  • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na kuwasalimia Watoto wa Mtaa wa Jangombe Wilaya ya Mjini Unguja leo 23-2-2024, baada ya kumaliza kumzungumza na Mzee Ramadhan Nzori
  • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na kumjulia hali yake Msanii Maarufu wa Zanzibar Bi.Mwapombe Hiyari, alipofika nyumbani kwake Chuini Wilaya ya Magharibi “A” Unguja leo 23-2-2024, ikiwa ni utaratibu wake kuwajulia hali Wazee mbalimbali Zanzibar.
  • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akijumuika na Familia ya Mzee Daudi Suleiman Ali, alipofika nyumbani kwake Fuoni Wilaya ya Magharibi “B” Unguja kwa ajili ya kumsalimia na kumjulia hali yake leo 23-2-2024.
  • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa katika mazungumzo na Mzee Ramadhan Nzori , aliyewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Jangombe Zanzibar, alipofika nyumbani kwake Jangombe Wilaya ya Mjini Unguja kwa ajili ya mazungumzo na kumjulia hali yake leo 23-2-2024