State House Blog

Dk.Shein akizungumza na Uongozi wa Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi

  • Viongozi katika Idara zilizochini ya Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi wakiwa katika mkutano wa utekelezaji wa mpango wa Kazi kwa mwaka wa Fedha wa 2017-2018, uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani).
  • Wasaidizi wa Rais wa Zanzibar wakiwa katika mkutano wa utekelezaji wa mpango wa Kazi kwa mwaka wa Fedha wa 2017-2018, kwa Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.
  • Katibu Mkuu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Dkt. Abduhamid Yahya Mzee(kulia) alipokuwa akichangia katika mkutano wa utekelezaji wa mpango wa Kazi kwa mwaka wa Fedha wa 2017-2018,kwa Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar (katikati) Waziri Issa Haji Ussi Gavu na (kushoto) Naibu Katibu Mkuu wa Baraza la Mapinduzi Nd,Salmin Amour Abdulla.
  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi katika kikao cha siku moja cha Utekelezaji wa Mpango kazi kwa kipindi cha robo ya kwanza Julai-Septemba 2017 kilichofanyika katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja.

Dk.Shein akutana na ujumbe wa Shirika la Help Age International.

  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Barazaa la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mwenyekiti wa Shirika la kuwahudumia Wazee Duniani "Help Age International" Bw.Arun Maura alipoongoza ujumbe aliofuatana nao ulipofika Ikulu Mjini Unguja.
  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Barazaa la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na Ujumbe wa Shirika la kuwahudumia Wazee Duniani "Help Age International" ulioongozwa na Mwenyekiti Bw.Arun Maura (wa pili kulia) wakati ulipofika Ikulu Mjini Unguja.

Sherehe za kutimiza miaka 72 ya Umoja wa Mataifa UN, tokea kuasisiwa

  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Barazaa la Mapinduzi Mheshimiwa Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akitoa hutuba yake wakati wa sherehe za kutimiza miaka 72 ya Umoja wa Mataifa UN, tokea kuasisiwa kwake zilizofanyika jana katika Hoteli ya Serena Mjini Zanzibar,
  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Barazaa la Mapinduzi Mheshimiwa Dk.Ali Mohamed Shein akiteta jambo na Mratibu Mkaazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo UNDP Nchini Tanzania Bw.Alvaro Rodriguez wakati wa sherehe za kutimiza miaka 72 ya Umoja wa Mataifa UN, tokea kuasisiwa kwake zilizofanyika katika Hoteli ya Serena Mjini Zanzibar
  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Barazaa la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mratibu Mkaazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo UNDP Nchini Tanzania Bw.Alvaro Rodriguez wakati alipowasili katika Hoteli ya Serena Zanzibar jana katika sherehe za Umoja wa Mataifa UN kutimiza miaka 72 tokea kuasisiwa kwake

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Barazaa la Mapinduzi Mheshimiwa Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akitoa hutuba yake wakati wa sherehe za kutimiza miaka 72  ya Umoja wa Mataifa UN, tokea kuasisiwa kwake zilizofanyika jana katika Hoteli ya Serena Mjini Zanzibar,
 

Dk.Shein akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Fedha na MipangoMipango   katika kikao cha Utekelezaji

  • Baadhi ya Viongozi wa Idara mbali mbali zilizo chini ya Wizara ya Fedha na Mipango wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,alipozungumza na Uongozi wa Wizara hiyo leo katika kikao cha siku moja cha Utekelezaji wa Mpango kazi kwa kipindi cha robo ya kwanza Julai- Septemba 2017 katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja
  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Fedha na Mipango katika kikao cha siku moja cha Utekelezaji wa Mpango kazi kwa kipindi cha robo ya kwanza Julai- Septemba 2017 kilichofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja

Dk.Shein, ameupongeza uongozi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali kwa kutekeleza majukumu yake

  • Baadhi ya Viongozi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali wakifuatilia kwa makini taarifa ya Utekelezaji wa Mpango kazi kwa kipindi cha robo ya kwanza Julai- Septemba 2017 iliyosomwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Nd,Khadija Bakari Juma(wa pili kushoto) katika kikao cha siku moja kilichofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja,chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani)
  • Baadhi ya Viongozi wa Idara mbali mbali katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali wakiwa katika kikao cha siku moja cha Utekelezaji wa Mpango kazi kwa kipindi cha robo ya kwanza Julai- Septemba 2017 kilichofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja,chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani),
  • Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe.Riziki Pembe Juma (kulia) akiwasilisha taarifa ya Utekelezaji wa Mpango kazi kwa kipindi cha robo ya kwanza Julai- Septemba 2017 katika kikao cha siku moja cha Uongozi wa Wizara hiyo kilichofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja,chini ya Mwenyekiti wake **Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) na (kushoto) Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe.Mmanga Mjengo Majawiri