Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt, Hussein Ali Mwinyi amesema Watanzania wana Wajibu muhimu wa kuhakikisha Muungano wa Tanzania Amani, Utulivu na Umoja wa kitaifa vinalindwa ,Kuimarishwa na Kudumishwa. Rais Dķt, ameyasema hayo leo tarehe 2 Aprili 2026 katika Uzinduzi wa Kitaifa wa Mbio za Mwenge wa Uhuru uliofanyika Uwanja wa Gombani, Mkoa wa Kusini ,Pemba.
Rais Dķt Mwinyi amefahamisha kuwa Serikali zote mbili ,Taasisi za Dini,Asasi za kiraia ,Vyombo vya Habari na Wananchi wana Wajibu wa kulinda Misingi ya Utu na kuheshimu Utawala wa Sheria ili kuwa na Taifa linalosimamia Haki,Usawa ,Umoja, ,Utulivu na Mshikamano wa kitaifa.
Ameeleza kuwa Mwenge wa Uhuru ni Chombo muhimu cha Kuhimiza Haki ,Usawa,,Umoja na Uwajibikaji katika Ujenzi wa Taifa sambamba kuangaza na kutokomeza Maadui Umasikini, Ujinga na Maradhi ikiwa ni Utekelezaji wa Dhamira ya Viongozi Waasisi wa Taifa la Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Mzee Abeid Amani Karume. Rais Dķt Mwinyi amesisitiza kuwa Amani, Umoja ,Utulivu na Mshikamano wa Kisiasa na kijamii ndio Msingi wa Maendeleo Endelevu ambapo Utulivu wa Nchi huwapa Viongozi fursa ya kuandaa Sera za Maendeleo Endelevu na kusimamia Utekelezaji wake kwa Ufanisi.
Aidha amefahamisha kuwa Sababu zote za Ubaguzi Matokeo yake ni Mabaya na yanaweza kusababisha hali ya Kutoami niana ,Utengano wa Kikabila ,kidini, Kisiasa au Kijiografia na hatimae Nchi kuingia katika Misuguano ambayo inaweza kusababisha Machafuko na Mgawanyiko Mkubwa katika Taifa.Amewahimiza Watanzania kuungana kupinga aina zote za Ubaguzi na kudumishab Umoja wa Kitaifa kwani ni wakati sahihi wa kuonesha Uzalendo kwa Taifa ,Kulinda Rasilimali na kuandaa na kujenga Kizazi kinachotanguliza mbele maslahi ya Taifa na kulilinda.
Rais Dķt, Mwinyi amevinasihi Vyama vya Siasa na Viongozi wake kutekeleza Majukumu yao kwa Kutanguliza Tanzania Kwanza pamoja na kuhakikisha Tunu ya Amani inalindwa Wakati wote na kuwasisitiza Wananchi kuunga mkono juhudi za Serikali za kupambana na rushwa hapa Nchi na kuwatayari kuwafichua Wale wote wanaojihusisha na Utoaji na upokeaji wa rushwa.
Akizungumzia Ugonjwa wa Ukimwi Rais Dkt Mwinyi amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zinaendeleza juhudi za Mapambano dhidi ya Ugonjwa huo kwa kuhakikisha Upatikanaji wa Dawa za ARV bila ya Malipo na kupunguza Vifo vinavyotokana na Ukimwi hadi kufikia 24,000 katika Mwaka 2024.
Kuhusiana na janga la Dawa za kulevya Rais Dkt, Mwinyi amesema Serikali zote mbili zimeendelea na kuimarisha Operesheni katika Mipaka ,Bandari na Viwanja vya Ndege na kutoa elimu hususani kwa Vijana ili kupunguza Matumizi ya dawa za kulevya .
Amefahamisha kuwa hadi kufikia Mwezi Disemba 2025 Waraibu 18,970 walipatiwa huduma za Tiba katika Vituo 16 vya Matibabu na zaidi ya Waraibu 19,000 wanahudumiwa katika Nyumba 77 za Upqtaji Nafuu pia Waraibu 728 walipatiwa huduma za Tiba katika kituo cha Tiba na Marekebisho ya Tabia cha Kidimni Zanzibar.
Akizungumzia Ugonjwa wa Malaria Rais Dkt, Mwinyi amesema Takwimu za Wizara ya Afya za Mwqka 2025 zinaonesha kuwa takriban asilimia 6.2 ( Wagonjwa Milioni 2.8 ya Wagonjwa wa nje(OPD) walithibitika kuwa na Malaria na Wagonjwa 199,347 waliolazwa Hosptali
Asilimia 11 wali na Malaria na wengi wao walikuwa Watoto chini ya Miaka Mitano na Mama Wajawazito.
Raiis Dkt, Mwinyi amesema pamoja na Ugonjwa huo kuwa sugu Serikaimepiga hatua kubwa katika kuudhibiti ambapo hadi kufikia Mwaka 2025,Kiwango cha Maambukizi kimepungua kutoka asilimia 8.1Mwaka 2022 hadi kufikia asilimia 5.5 Mwaka 2025.
Amesema Serikali imechukua juhudi mbalimbali za kupambana na Malaria kwq kusambaza Vyandarua vyenye Dawa,Udhibiti wa Mazalia ya Mbu na kuimarisha huduma za Uchunguzi wa Matibabu pamona na kutenga Shilingi Bilioni10 za kununua zaidi ya Lita 833,000 za Vidudu vya Kibailojia vilivyosambazwa katika Halmashauri 184 na Upatikqnaji waVipimo vya Dawa kufikia zaidi ya asilimia 90 katika Vituo vya Afya.
Tayari Mwenge wa Uhuru umeanza kukimbizwa rasmi katika Visiwa vya Zanzibar.
