Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ameshiriki hafla ya uapisho wa Waziri Mkuu Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, ambaye ameapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan. Hafla hiyo imefanyika leo, tarehe 14 Novemba 2025, Ikulu Chamwino.
Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba ameteuliwa hivi karibuni baada ya jina lake kupendekezwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, na baadaye kupigiwa kura na Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jana, tarehe 13 Novemba 2025.
Hafla hiyo imehudhuriwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Emmanuel Nchimbi, pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali wastaafu na waliopo madarakani kutoka SMT na SMZ, Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, viongozi wa vyama vya siasa, vyombo vya ulinzi na usalama, viongozi wa dini, na wageni waalikwa.
Rais Dkt. Mwinyi amewasili leo tarehe 14 Novemba 2025, Dodoma akitokea Zanzibar kwa ajili ya hafla hiyo pamoja na Uzinduzi wa Bunge la 13 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
