Media » News and Events

Dk. Hussein Ali Mwinyi ametoa salamu za rambirambi kwa familia za marehemu waliofariki kufuatia kula samaki wa kasa anayesadikiwa kuwa na sumu.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi ametoa salamu za rambirambi kwa familia za marehemu waliofariki kufuatia kula samaki wa kasa anayesadikiwa kuwa na sumu huko katika kijiji cha Msuka Taponi, Wilaya ya Micheweni, Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Katika salamu hizo za rambirambi,  Rais Dk. Mwinyi alieleza kusikitishwa na vifo hivyo na kuzitaka familia za marehemu hao kuwa na subira na ustahamilivu katika kipindi hiki kigumu cha misiba hiyo.Rais Dk. Mwinyi alimuomba Mwenyezi Mungu awalaze Marehemu wote mahala pema peponi,  Amin.

Aidha, Rais Dk. Mwinyi amemuomba MwenyeziMungu kuwaponesha kwa haraka waliodhurika baada ya kula samaki huyo anayesadikiwa kuwa na sumu.Rais Dk. Mwinyi katika salamu zake hizo la pole,alisema kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara yake husika itaendelea kuhakikisha Wale wote waliodhurika wanaendelea kupatiwa tiba sahihi ili waweze kurudi katika hali nzuri za kiafya.