Ikulu Blog

Rais wa Zanzibar Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi ametowa Mkono wa Eid Fitry kwa Wananchi katika viwanja vya Ikulu Zanzibar.

  • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akiitikia dua ikisomwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi, baada ya kumaliza mazungumzo na Masheikh wa Zanzibar walipofika Ikulu Jijini Zanzibar kwa kumsalimia leo 3-5-2022, baada ya kumaliza kwa Sala ya Eid Fitry iliyofanyika Masjid Jamiu Zinjibar Mazizini Unguja Jijini Zanzibar.
  • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria, Utumishi na Utawala Bora Zanzibar Mhe.Haroun Ali Suleiman, baada ya kumaliza mazungumzo yake na Masheikh wa Zanzibar Ikulu Zanzibar.
  • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akitowa mkono wa Eid Fitry kwa Watoto waliofika viwanja vya Ikulu Jijini Zanzibar kwa ajili ya kupokea Mkono wa Eid Fitry, baada ya kumalizika kwa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.
  • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Masheikh wa Zanzibar, baada ya kumaliza Sala ya Eid Fitry iliyofanyika katika Masjid Jamiu Zinjibar Mazizini Unguja, mazungumzo hayo yaliofanyika Ikulu Jijini Zanzibar, walipofika kumsalimia leo 3-5-2022.

Rais wa Zanzibar Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi amelihutubia Baraza La Eid Fitry Ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Unguja Jijini Zanzibar.

  • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akipokea salamu ya heshima kutoka Kikosi cha Jeshi la Polisi cha FFU gwaride maalumu lilioandaliwa kwa ajili ya Baraza la Eid Fitry katika viwanja vya ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Unguja Jijini Zanzibar.
  • BAADHI ya Mawaziri na Wageni waalikwa katika hafla ya Baraza la Eid Fitry wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi.(hayupo pichani) akilihutubia katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Unguja Jijini Zanzibar.
  • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akipokea salamu ya heshima kutoka Kikosi cha Jeshi la Polisi cha FFU gwaride maalumu lilioandaliwa kwa ajili ya Baraza la Eid Fitry katika viwanja vya ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Unguja Jijini Zanzibar leo 3-5-2022.
  • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akifuatilia tafsiri ya maelezo mafupi ya Aya Suratul-Fat’hi wakati wa hafla ya Baraza la Eid Fitry lililofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Unguja na (kushoto kwa Rais) Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi na (kulia kwa Rais) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria,Utumishi na Utawala Bora Zanzibar Mhe.Haroun Ali Suleiman.

Rais wa Zanzibar Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi amejumuika na waumini wa Dini ya Kiislam katika Sala ya Eid Elfity Masjid Jamiu Zinjibar Mazizini Zanzibar.

  • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akijumuika na Waumini wa Dini ya Kiislam katika Sala ya Eid Fitry iliyofanyika leo asubuhi katika Masjid Jamiu Zinjibar Mazizini Unguja Jijini Zanzibar.
  • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Viongozi wa Serikali na Dini baada ya kuwasili katika Masjid Jamiu Zinjibar Mazizini Unguja kuhudhuria Sala ya Eid Fitry baada ya kumalizika kwa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, Sala hiyo iliyofanyika katika Masjid hiyo leo 3-4-2022.
  • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa katika viwanja vya Masjid Jamiu Zinjibar Mazizini Unguja wakati ikipingwa mizinga baada ya kumalizika kwa Sala ya Eid Fitry iliyofanyika katika Masjid hiyo na (kulia kwa Rais) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria, Utumishi na Utawala Bora Mhe.Haroun Ali Suleiman na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Idrisa Mustafa Kitwana na (kushoto kwa Rais) Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla.

Rais wa Zanzibar ambae ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amepiga kura Shina namba moja Tawi la Kilimani Unguja.

  • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambae ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akipiga kura yake katika Shina namba moja Tawi Chama Cha Mapinduzi Kilimani Shehia ya Kilimani Unguja kumchagua Mwenyekiti wa Shina na Wajumbe, uchaguzi huo uliofanyika katika Tawi hilo Migombani 22-4-2022.
  • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambae ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Wananchama wa Shina namba moja Tawi la CCM Kilimani Unguja, baada ya kumaliza kupiga kura yake kumchangua Mwenyekiti na Wajumbe wa Shina namba moja Tawi la CCM Kilimani Unguja uliofanyika 22-4-2022.na (kulia kwa Rais) Mbunge wa Jimbo la Mpendae Zanzibar Mhe Toffiq Salim Turky.

Mke wa Rais Wa Zanzibar ambae ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Mama Mariam Mwinyi ametoa Sadaka ya Futari kwa Wazee,Wajane na wenye hali ngumu Tumbatu.

  • MKE wa Rais wa Zanzibar ambae ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Mama Mariam Mwinyi akisalimiana na kuagana na Wazee wa Tumbatu baada ya kumalizika kwa hafla ya kutoa Sadaka ya Futari kwa Wajane Wazee na Wenye Hali Ngumu katika Kisiwa cha Tumbatu Mkoa wa Kaskazini Unguja leo 21-4-2022.
  • MKE wa Rais wa Zanzibar ambae ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora. Mama Mariam Mwinyi akimabidhi mmoja wa Wazee wa Tumbatu Sadaka ya Futari Bi.Tabu Kheri Haji ikiwa ni moja ya vyakula alivyokabidhiwa kwa Wajane Wazee na Wenye hali ngumu, hafla hiyo iliyofanyika katika Kijiji cha Jongowe Tumbatu Unguja leo 21-4-2022.
  • WAZEE wa Tumbatu wakimsikiliza Mke wa Rais wa Zanzibar ambae ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Mama Mariam Mwinyi.(hayupo pichani) wakati wa hafla ya kutoa Sadaka ya Futari kwa Wajane Wazee na Wenye hali Ngumu iliyofanyika katika Kijiji cha Jongowe Tumbatu Mkoa wa Kaskazini Unguja leo 21-4-2022.
  • MKE wa Rais wa Zanzibar ambae ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Mama Mariam Mwinyi akiitikia ikisomwa na Sheikh.Makame Said Khamis.(hayupo pichani) baada ya kumalizika kwa hafla ya kutoa Sadaka ya Futari kwa Wajane Wazee na Wenye Hali Ngumu katika Kisiwa cha Tumbatu, iliyofanyika katika Kijiji cha Jongowe na (kulia kwake) Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe.Ayoub Mohammed Mahmoud na (kushoto kwake) Sheha wa Shehia ya Jongowe Bi. Miza Ali Sharif.
  • MKE wa Rais wa Zanzibar ambae ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Mama Mariam Mwinyi akielekea katika eneo lililoandaliwa kwa ajili ya kutoa Sadaka ya Futari kwa Wajane Wazee na Wenye hali ngumu katika Kisiwa cha Tumbatu na (kulia kwake) Sheha wa Shehia ya Jongowe Bi.Miza Ali Sharif na (kushoto kwake) Mkurugenzi wa Jumuiya ya Wajane Zanzibar Bi.Tabia Makame.
  • MKE wa Rais wa Zanzibar ambae ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Mama Mariam Mwinyi akisalimiana na Sheha wa Shehia ya Tumbatu Jongowe Bi.Miza Ali Sharif, alipowasili katika Kisiwa cha Tumbatu kwa ajili ya hafla ya kutoa Sadaka ya Futari kwa Wajane Wazee na Wenye hali ngumu, hafla hiyo imefanyika katika Kijiji cha Jongowe Tumbatu.
  • MKE wa Rais wa Zanzibar ambae ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Mama Mariam Mwinyi akisalimiana na Viongozi wa Mkoa wa Kusini Wilaya ya Kati Unguja baada ya kuwasili katika viwanja vya Skuli ya Msingi Uzi,kwa ajili ya kutoa Sadaka ya Futari kwa Wazee kuazia umri wa miaka 70 wa Shehia mbili za Uzi na Ngambwa na (kushoto kwake) Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Mhe Rashid Hadidi.
  • MKE wa Rais wa Zanzibar ambae ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Mama Mariam Mwinyi akizungumza na kutowa nasaha zake kwa Wananchi wa Uzi, wakati wa hafla ya kutoa Sadaka ya Futari kwa Wazee wa umri wa miaka 70, hafla hiyo iliyofanyika katika Skuli ya Msingi Uzi na (kushoto kwake) Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Mhe.Rashid Hadidi.
  • MKE wa Rais wa Zanzibar ambae ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Mama Mariam Mwinyi akimkabidhi mmoja wa Wazee wa Kijiji cha Uzi Sadaka ya Futari, aliyokabidhi kwa Wazee wa Shehia mbili za Uzi na Ngambwa , hafla hiyo iliyofanyika katika Skuli ya Msingi Uzi Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
  • MKE wa Rais wa Zanzibar ambae ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Mama Mariam Mwinyi akimkabidhi Misahafu Sheikh Ali Othman kwa ajili ya Madrasa na Misikiti ya Shehia ya Uzi na Ngambwa, hafla hiyo iliyofanyika katika Skuli ya Msingi Uzi.