RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akilihutubia Baraza la Eid Al Hajj, lililofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Amali Mkokotoni Mkoa wa Kaskazini Unguja
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akilihutubia Baraza la Eid Al Hajj, lililofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Amali Mkokotoni Mkoa wa Kaskazini Unguja 10-7-2022, na kuhudhuria na Viongozi mbalimbali wa Serikali, Wananchi na wa Vyama vya Siasa Zanzibar.
Rais wa Zanzibar Dk.Hussein Ali Mwinyi amefika nyumbani kwa mfanyakazi wake kutoa mkono wa pole.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi (katikati) leo amefika Nyumbani kwa Mfanyakazi wake kutoa mkono wa pole baada ya kifo cha Baba Mzazi wa Mfanyakazi huyo huko nyumbani kwao Dole,Ndunduke Wilaya ya Magharibi"A" Mkoa wa Mjini Magharibi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi (katikati) akisalimiana na wanafamilia wa Marehemu Bw.Mohamed Ali Juma mume wa Mbunge wa Jimbo la Bububu Mhe.Mwantakaje Haji Juma alipofika Nyumbani kwao Bububu Kijichi Wilaya ya Magharibi"A" Mkoa wa Mjini Magharibi kutoa mkono wa pole.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi (katikati) alipofika Nyumbani kwa Mbunge wa Jimbo la Bububu Mhe.Mwantakaje Haji Juma (wa pili kulia) leo kutoa Mkono wa pole baada ya kufiliwa na mume wake Marehemu Mohamed Ali Juma, Kijichi Wilaya ya Magharibi"A" Mkoa wa Mjini Magharibi.
Rais Dk.Mwinyi ameshiriki swala ya Ijumaa Msikiti wa Miembeni Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi (katikati) leo ameshiriki katika swala ya Ijumaa katika Msikiti wa Miembeni Jijini Zanzibar iliyoswalishwa na Sheikh Iddi Muhsin Iddi kutoka Ofisi ya Muftiu Mkuu wa Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi (kushoto) akiagana na Spika wa baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe.Zubeir Ali Maulid (katikati)pamoja Viongozi wengine mara baada ya Swala ya Ijumaa ilyoswaliwa leo katika msikiti wa Miembeni Jijini Zanzibar.
Baadhi ya Waumini wa Dini ya kiislamu wakiwa katika Msikiti wa Miembeni Jijini Zanzibar wakisikiliza hutba ya swala ya Ijumaa katika Msikiti wa Miembeni Jijini Zanzibar iliyosomwa na Sheikh Khalid Ali Mfaume (hayupo picnani), na swala ikaswalishwa na Sheikh Iddi Muhsin Iddi kutoka Ofisi ya Muftiu Mkuu wa Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi (wa tatu kulia) pamoja Viongozi wengine wakiitikia dua Iliyoombwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi,(katikati) baada ya Swala ya Ijumaa ilyoswaliwa katika msikiti wa Miembeni Jijini Zanzibar.
Mke wa Rais Wa Zanzibar ambae ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation Mama Mariam Mwinyi amekabidhiwa msaada wa Vifaa kwa ajili ya utengenezaji wa Sabuni ya mwani kwa wanawake.
MKE wa Rais wa Zanzibar ambae ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation Mama Mariam Mwinyi akikabidhiwa glovzi kwa ajili ya matumizi ya utengenezaji wa sabuni ya mwani na Meneja wa Kampuni ya CRJE Tawi la Zanzibar Bw. Shi.Yan, hafla hiyo ya kukabidhi msaada huo wa vifaa mbalimbali vilivyotolewa na Kampuni ya CRJE kwa ajili ya Vikundi vya Wanawake wa Kilimo cha Mwani Zanzibar, iliyofanyika katika Ofisi za Taasisi hiyo Migombani Unguja.
MKE wa Rais wa Zanzibar ambe ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation Mama Mariam Mwinyi akiangalia kifaa kwa ajili ya utengeneza sabuni, baada ya kukabidhiwa na Meneja wa Kampuni ya CRJE Tawi la Zanzibar Bw.Shi Yan (kulia) kwa ajili ya Vikundi vya Wajasiriamali wa Mwani Zanzibar.
MKE wa Rais wa Zanzibar ambae ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation Mama Mariam Mwinyi akikabidhiwa mashine ya kuchanganya ungwa wa mwani kwa ajili ya utengenezaji wa sabuni na Meneja wa Kampuni ya CRJE Bw.Shi Yan, hafla hiyo ya kukabidhi vifaa hivyo uliofanyika katika Ofisi za Taasisi hiyo migombani Unguja.
MKE wa Rais wa Zanzibar ambae ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation Mama Mariam Mwinyi akizungumza na ujumbe wa Kampuni ya CRJE, walipofika katika Ofisi za Taasisi hiyo migombani Unguja kwa ajili ya kukabidhi msaada wa Vifaa vya utengenezaji wa Sabuni ya Mwani kwa ajili ya Vikundi vya Wajasiriamali wa bidhaa za mwazi Zanzibar.
Rais wa Zanzibar Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amekutana na kuzungumza na Balozi wa Oman Nchini Tanzania Ikulu Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Balozi wa Oman Nchini Tanzania Mhe.Saud Hilal Al Shidhani.(kulia kwa Rais) alipofika Ikulu kwa mazungumzo na kujitambulisha akiwa na Balozi Mdogo wa Oman anayefanyia Kazi zake Zanzibar Mhe.Said Salim Al Sinawi,mazungumzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiagana na mgeni wake Balozi wa Oman Nchini Tanzania Mhe.Saud Hilal Al Shidhani.(kulia kwa Rais) baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyia katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar, alipofika kujitambulia akiwa na Balozi Mdogo wa Oman anayefanyika kazi zake Zanzibar Mhe.Said Salim Al Sinawi.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Balozi wa Oman Nchini Tanzania Mhe.Saud Hilal Al Shidhani.(kulia kwa Rais) alipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo na kujitambulisha akiwa na Balozi Mdogo wa Oman anayefanyia Kazi zake Zanzibar Mhe.Said Salim Al Sinawi na Ujumbe wake, mazungumzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Balozi wa Oman Nchini Tanzania Mhe.Saud Hilal Al Shidhani, alipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo na kujitambulisha mazungumzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar.