Mke wa Rais Wa Zanzibar ambae ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation Mama Mariam Mwinyi amekabidhiwa msaada wa Vifaa kwa ajili ya utengenezaji wa Sabuni ya mwani kwa wanawake.
MKE wa Rais wa Zanzibar ambae ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation Mama Mariam Mwinyi akikabidhiwa glovzi kwa ajili ya matumizi ya utengenezaji wa sabuni ya mwani na Meneja wa Kampuni ya CRJE Tawi la Zanzibar Bw. Shi.Yan, hafla hiyo ya kukabidhi msaada huo wa vifaa mbalimbali vilivyotolewa na Kampuni ya CRJE kwa ajili ya Vikundi vya Wanawake wa Kilimo cha Mwani Zanzibar, iliyofanyika katika Ofisi za Taasisi hiyo Migombani Unguja.
MKE wa Rais wa Zanzibar ambe ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation Mama Mariam Mwinyi akiangalia kifaa kwa ajili ya utengeneza sabuni, baada ya kukabidhiwa na Meneja wa Kampuni ya CRJE Tawi la Zanzibar Bw.Shi Yan (kulia) kwa ajili ya Vikundi vya Wajasiriamali wa Mwani Zanzibar.
MKE wa Rais wa Zanzibar ambae ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation Mama Mariam Mwinyi akikabidhiwa mashine ya kuchanganya ungwa wa mwani kwa ajili ya utengenezaji wa sabuni na Meneja wa Kampuni ya CRJE Bw.Shi Yan, hafla hiyo ya kukabidhi vifaa hivyo uliofanyika katika Ofisi za Taasisi hiyo migombani Unguja.
MKE wa Rais wa Zanzibar ambae ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation Mama Mariam Mwinyi akizungumza na ujumbe wa Kampuni ya CRJE, walipofika katika Ofisi za Taasisi hiyo migombani Unguja kwa ajili ya kukabidhi msaada wa Vifaa vya utengenezaji wa Sabuni ya Mwani kwa ajili ya Vikundi vya Wajasiriamali wa bidhaa za mwazi Zanzibar.
Rais wa Zanzibar Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amekutana na kuzungumza na Balozi wa Oman Nchini Tanzania Ikulu Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Balozi wa Oman Nchini Tanzania Mhe.Saud Hilal Al Shidhani.(kulia kwa Rais) alipofika Ikulu kwa mazungumzo na kujitambulisha akiwa na Balozi Mdogo wa Oman anayefanyia Kazi zake Zanzibar Mhe.Said Salim Al Sinawi,mazungumzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiagana na mgeni wake Balozi wa Oman Nchini Tanzania Mhe.Saud Hilal Al Shidhani.(kulia kwa Rais) baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyia katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar, alipofika kujitambulia akiwa na Balozi Mdogo wa Oman anayefanyika kazi zake Zanzibar Mhe.Said Salim Al Sinawi.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Balozi wa Oman Nchini Tanzania Mhe.Saud Hilal Al Shidhani.(kulia kwa Rais) alipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo na kujitambulisha akiwa na Balozi Mdogo wa Oman anayefanyia Kazi zake Zanzibar Mhe.Said Salim Al Sinawi na Ujumbe wake, mazungumzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Balozi wa Oman Nchini Tanzania Mhe.Saud Hilal Al Shidhani, alipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo na kujitambulisha mazungumzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar.
Rais wa Zanzibar Mhe.Dk.Hussein Mwinyi amezungumza baada ya kuwaapisha Viongozi aliowateua hivi karibuni
VIONGOZI Wakuu wa Serikali wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi.(hayupo pichani) akihutubia baada ya kumaliza kuwaapisha Viongozi aliowateua hivi karibuni (kutoka kulia) Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe.Othman Masoud Othman, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla,Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe Zuberi Ali Maulid na Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe Khamis Ramadhan Abdalla.
Rais wa Zanzibar Dkt.Hussin Ali Mwinyi ameondoka nchini Burundi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi akifuatana na Mkewe Mama Mariam Mwinyi pamoja na Maafisa mbali mbali wakati akiondoka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar, akiagana na Mawaziri na Viongozi mbali mbali wakati akiondoka kuelekea nchini Burundi kuhudhuria sherehe za maiaka 60 ya nchi hiyo akimuakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Mama Samia Suluhu Hassan.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi akiagana na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemedi Suleiman katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar, akiondoka kuelekea nchini Burundi kuhudhuria sherehe za maiaka 60 ya nchi hiyo akimuakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Mama Samia Suluhu Hassan.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi akiteta na Katibu wa Baraza la Mapinduzi pia Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar, akiondoka kuelekea nchini Burundi kuhudhuria sherehe za miaka 60 ya nchi hiyo akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Mama Samia Suluhu Hassan,(kulia) Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemedi Suleiman.
Rais Dkt.Hussein Ali Mwinyi amemuapisha Jaji Mkuu wa Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi (kushoto) akimuapisha Mhe.Khamis Ramadhan Abdalla (kulia)kuwa Jaji Mkuu wa Zanzibar katika hafla iliyofanyika leo katika Ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar kabla uteuzi alikaimu nafasi hiyo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi (kushoto) akimuapisha Mhe.Said Hassdan Said (kulia)kuwa Jaji wa Mahkama Kuu ya Zanzibar katika hafla iliyofanyika leo Ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar kabla alikuwa Mwanasheria Mkuu Awamu ya 7 Uongozi uliopita.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi (kushoto) akimuapisha Mhe.Salma Ali Hassan (kulia)kuwa Jaji wa Mahkama Kuu ya Zanzibar katika hafla iliyofanyika leo Ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar kabla alikuwa Mkurugenzi Mashtaka Zanzibar .
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi (kushoto) akimuapisha Mhe.Mohamed Ali Mohamed (kulia)kuwa Jaji wa Mahkama Kuu ya Zanzibar katika hafla iliyofanyika leo Ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibarkabla alikuwa Mrajis wa Mahkama Kuu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe.Haroun Ali Suleiman na Viongozi wengine ni miongoni mwa Waalikwa waliohudhuria katika hafla ya kuapishwa Majaji wa Mahkama Kuu wa Zanzibar katika Ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.
Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Dkt.Mwinyi Talib Haji (kulia) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu Mhe.Jamal Kassim Ali na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said ni miongoni mwa Viongozi waliohudhuria katika hafla ya kuapishwa Majaji wa Mahkama Kuu wa Zanzibar leo katika Ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.
Baadhi ya Wageni walioalikwa katika hafla ya kuapishwa Majaji wa Mahkama Kuu wa Zanzibar leo katika Ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.
Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama Zanzibar wakishuhudia Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akiwaapisha Majaji wa Mahkama Kuu ya Zanzibar hafla iliyofanyika leo Ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.
Majaji wa Mahkama Kuu ya Zanzibar wakishuhudia kuapishwa kwa Majaji wapya walioteuliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) katika hafla iliyofanyika leo Ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.