State House Blog

Rais wa Zanzibar Alhajj Dk. Hussein Ali Mwinyi ameongoza wananchi katika kisoma cha dua Maalum kumuombea Rais wa kwanza wa Zanzibar

 • VIONGOZI wa Dini na Waumini wa Kiislam wakisoma hitma na dua kumuombea Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Marehemu Abeid Amani Karume, kisomo hicho kimefanyika katika ukumbi wa Afisi Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Kisiwandui Jijini Zanzibar
 • MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akitia ubani wakati wa hafla ya kisoma cha Dua na Hitma ya kumuombea Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Marehemu Abeid Amani Karume na (kulia) kwake ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, kisomo hicho kimefanyika katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Jijini Zanzibar.
 • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akiongoza kisoma cha Dua na Hitma ya kumuombea Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Marehemu Abeid Amani Karume, iliofanyika katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Jijini Zanzibar na (kulia kwa Rais) ni Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi na Waziri Mkuu wa Tanzania Alhajj Kassim Majaliwa na (kushoto kwa Rais) Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Hassan Othman Ngwali, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman
 • RAIS wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akiitikia dua ya kuhitimisha kisomo cha hitma ikisomwa na Bi.Maryam Mliwa (kulia) Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi na Mke wa Makamu wa Kwanza wa Rais Mama Zuhura Kassim na (kulia kwa Rais) Mke wa Makamu wa Pili wa Rais Mama Sharifa Omar Khalfan. Wakiitikia dua
 • MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman,Rais Mstaaf wa Zanzibar Alhajj Dkt. Amani Karume, Makamu wa Rais Mstaaf wa Tanzania Alhajj Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Makamu wa Pili wa Rais Mstaaf Alhajj Balozi Seif Ali Iddi na Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu wakiitikia dua katika hafla ya kisomo cha Hitma na Dua iliofanyika katika ukumbi wa Afisi Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Kisiwandui Zanzibar
 • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akiitikia dua ikisoma na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi (kulia kwa Rais) na Waziri Mkuu wa Tanzania Alhajj Kassim Majaliwa na (kushoto kwa Rais) Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Hassan Othman Ngwali
 • MJANE wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Marehemu Abeid Amani Karume,MAMA Fatma Karume akishiriki katika kisomo cha Dua na Hitma ya kumuombea marehemu iliofanyika katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Jijini Zanzibar na (kulia) Mke wa Rais Mstaa wa Zanzibar Mama Shadya Karume na Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe.Mgeni Hassan Juma.
 • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akiweka shada la maua katika kaburi la Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Marehe Abeid Amani Karume, baada ya kumalizika kwa kisomo maalum na dua iliofanyika katika ukumbi wa Afisi Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Kisiwandui Jijini Zanzibar.
 • MUFTI Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi akisoma dua baada ya kumalizika kwa kisomo cha hitma ya kumuombea Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Marehemu Abeid Amani Karume na (kushoto kwake) Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk. Hussein Ali Mwinyi na (kulia) Waziri Mkuu wa Tanzania Alhajj Kassim Majaliwa.
 • MWAKILISHI wa Familia ya Marehemu Mzee Abeid Amani Karume Balozi Ali Karume akiweka shada la maua katika kaburi la marehemu viwanja vya Afisi Kuu ya CCM Kisiwandu Jijini Zanzibar
 • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akiweka shada la maua katika kaburi la Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Marehe Abeid Amani Karume, baada ya kumalizika kwa kisomo maalum na dua iliofanyika katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Jijini Zanzibar
 • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi,Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu wa Tanzania Alhajj Kassim Majaliwa, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe.Othman Masoud Othman, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Idrisa Musta Kitwana wakiitikia dua ikisomwa na Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar sheikh. Othman Hassan Ngwali katika kaburi la Marehemu Abeid Amani Karume
 • MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi na (kulia kwake) Mama Fatma Karume na (kushoto kwake) Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said, wakiwa katika viwanja vya kaburi la Marehemu Abeid Amani Karume wakati wa kumuombea dua
 • RAIS wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan akiweka shada la maua katika kaburi la Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Marehemu Abeid Amani Karume, katika viwanja vya Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Jijini Zanzibar.