Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt. Hussein Ali Mwinyi, akisoma kisomo cha khitima pamoja na Wananchi katika Msikiti wa Jamia Zinjibar, Mazizini, Mkoa wa Mjini Magharibi baada ya kuungana na waumini wa Dini ya Kiislamu katika Khitmah ya kaka yake marehemu Abbas Ali Mwinyi iliyofanyika Msikiti hapo leo tarehe 27 Septemba, 2025. Hitma hiyo imeambatana pia na sadaka ya chakula kwa waumini waliohudhuria hafla hiyo.