Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dkt, Hussein Ali Mwinyi ametoa wito kwa Wanasiasa nchini kuyatumia Majukwaa ya Kampeni Kuhubiri Umoja na Mshikamano wa Wananchi.Alhaj Dkt, Mwinyi ameyasema hayo katika Dua Maalum ya Kuwaombea Viongozi Wakuu wa Kitaifa na Taifa ilioandaliwa na Madrassat Swifat Nnabawiyatil Karimah (MSOLOPA) cha Kilimani.     

Alhaj Dkt, Mwinyi amesema sio jambo jema kwa Wanasiasa kuhubiri Chuki na Mifarakano isio na Tija katika jamii. Aidha ametoa rai kwa Wagombea wa Vyama vyote vilivyopata Uteuzi wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) kuhubiri Amani kwanza na baadae kutangaza Sera za Vyama vyao kwa Wananchi.               

Alhaji Dkt, Mwinyi ameushukuru Uongozi wa Chuo hicho kwa Uamuzi wa kuandaa Dua hiyo ya Kuwaombea Rais wa Zanzibar na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, Samia Suluhu Hassan kwa kufanya jambo jema.Rais Dkt Mwinyi amechangia Shillingi Milioni 50 kwa ajili ya kuendeleza Ujenzi wa Chuo hicho na kutoa wito kwa Wananchi na Waumini kuunga mkono dhamira hiyo.     

Chuo cha Swifat Nnabawiyatil Karimah maarufu Msolopa kinaendelea Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 50 tangu kuanzishwa kwake Mwaka 1975 pamoja na Mazazi ya Mtume Muhammad (S.A.W)