Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt, Hussein Ali Mwinyi amesema lengo kuu la Serikali ya Awamu ya nane ni kufanya Mageuzi makubwa katika Sekta ya Michezo kwa kujenga Viwanja vya Kisasa ili kuibua Vipaji na kufundisha Wataalamu wa michezo mbalimbali.Rais Dkt, Mwinyi ameyasema hayo alipokifungua kiwanja cha Kisasa cha Michezo Kiliopo Kitope, Mkoa wa Kaskazini Unguja.   

Ameeleza kuwa Awamu ya kwanza ya Ujenzi wa Viwanja vya Michezo imevuka Ilani ya CCM ya 2020 -2025 kwa kiasi Kikubwa kwa Ujenzi wa Viwanja vya Mikoa na Wilaya.Rais Dkt Mwinyi amesema lengo ni kuona kila kipaji Kinaonekana ,Kukuzwa na kuendelezwa.

Rais, Dkt, Mwinyi amesema Serikali kupitia Wizara ya Michezo inaishajihisha jamii kushiriki Michezo yote ya Kisasa na Ile ya Asili ikiwemo ‘drafts’, Bao,Karata,Mchezo wa Ng’ombe,Baskeli na Resi za Ngalawa ili kurithisha Vizazi vijavyo, kutoa burudani,Kuenzi na Kudumisha Utamaduni.

Rais Dkt Mwinyi ameeleza kuwa Vipaji vinavyoandaliwa ni kuiwezesha Nchi kupata fursa ya kushiriki Mashindano ya Kikanda na Kimataifa na kuufikia Utalii wa Michezo na kuvutia wageni kutoka Nje pamoja na Michezo kuzalisha Ajira kwa Vijana. Amesema Serikali itaendelea kutoa fursa kwa Makundi yote ikiwemo Vijana,Wanawake na Watu wenye ulemavu Kushiriki Michezo katika Mazingira Rafiki na yenye Usalama Zaidi. 

Amebainisha kuwa Serikali inafahamu Changamoto zinazokumba Makundi hayo pale wanapotaka kushiriki Michezo kwa kukosekana kwa Mazingira rafiki, Umbali wa kufuata Viwanja vya Michezo na Udhalilishaji kwa Wanawake hali inayosababisha makundi hayo Kukosa Michezo hivyo Viwanja vinavyojengwa sasa vitamaliza changamoto hizo na makundi hayo kushiriki Michezo.

Rais Dkt Mwinyi ametoa wito kwa Uongozi wa Wizara ya Michezo ,Mashirikisho Taasisi za michezo ,Wadau na Vyama vya Michezo kuifanya Michezo kuwa jumuishi na shirikishi na nyenzo ya Kuhimizana Amani na Utulivu wa Nchi.Rais Dkt, Mwinyi amesema Miundombinu bora ya Michezo ndio Chachu muhimu ya kuibua Vipaji vya Vijana na Serikali imejizatiti kukabiliana na Changamoto zote za kimichezo ikiwemo soka na Michezo mengine katika ngazi ya Kikanda na Kimataifa.   

Rais Dkt,Mwinyi ameeleza kuwa Nchi inajivunia kuimarika kwa Miundombinu ya kisasa ya Michezo.Ameeleza kuwa Zanzibar imebahatika kuwa Mwenyeji wa Michuano ya Chan iliomalizika hivi Karibuni na inatarajiwa kuwa Mwenyeji wa Afcon mwaka 2027 hivyo maandalizi mazuri yanahitajika na Serikali imepanga Kujenga Viwanja vipya vyenye hadhi. 

Azma ya kufikia dhamira hiyo Serikali imefanya Ukarabati Mkubwa wa Uwanja wa New Amani Complex na Mao Tse Tung kwa Unguja na Gombani Pemba na inajenga Uwanja mpya Utakaochukua Mashabiki 21,000 Kizimkazi,Mkoa wa Kusini Unguja na Uwanja mpya utakaochukua Mashabiki 31,000 Fumba Mkoa wa Mjini Magharibi na Ujenzi wa Viwanja 17 kila Mkoa na Wilaya Unguja na Pemba.     

Rais Dkt Mwinyi ametoa wito kwa Uongozi wa Wizara ya Michezo ,Mashirikisho Taasisi za michezo ,Wadau na Vyama vya Michezo kuifanya Michezo kuwa jumuishi na shirikishi na nyenzo ya Kuhimizana Amani na Utulivu wa Nchi.