Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar na Mgombea Mteule wa CCM kwa nafasi ya Urais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ameshiriki Uzinduzi wa Kampeni za Chama Cha Mapinduzi iliyofanyika katika viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe, jijini Dar es Salaam leo tarehe 28 Agosti 2025.
Kampeni hizo zimezinduliwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Taifa, ambaye pia ni Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya CCM, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akiwa na Mgombea Mwenza, Dkt. Emmanuel John Nchimbi.
Pia Dkt.Mwinyi amekabidhiwa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2025-2030 na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Taifa, Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan.