Mgombea wa nafasi ya Rais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi ametoa Wito kwa Wazanzibari kuepuka Siasa za Kikanda, kidini , Ubaguzi na Mifarakano ili Nchi ipate Maendeleo zaidi.Rais Dkt, M winyi amesema hayo alipozungumza na Wananchi Katika Mkutano wa Kampeni uliofanyika Makombeni ,Wilaya Mkoani ,Mkoa wa Kusini Pemba.
Amesema Chama cha Mapinduzi kitaendelea kudumisha Amani ,Umoja ,Maridhiano na Mshikamano ili Serikali iweze kutekeleza mipango zaidi ya Maendeleo yenye manufaa kwa kila Mwananchi.Rais Dkt, amewahakikishia Wananchi kasi ya Maendeleo iliofanyika miaka mitano iliopita Itaongezeka zaidi kwa Mambo makubwa ya Maendeleo.
Akizungumzia Sekta ya Afya amesema Awamu ijayo Serikali inakuja na Mpango kwa Hospitali zote hapa nchini kuwa na Matibabu ya Kibingwa ikiwemo Hosptali ya Abdalla Mzee kuwa na Mashine ya MRI.Akizungumzia Miundombinu amesema Uzinduzi wa Ujenzi wa Ndege wa Pemba na Barabara ya Chakechake-Mkoani kunalenga Kuifungua Pemba Kiuchumi na kuwa na Maendeleo zaidi.
Rais Dkt, Mwinyi ameeleza, kuwa Suala la Ajira kwa Vijana ni kipaumbele cha Kwanza kwa Awamu Ijayo na kuwa Serikali itahakikisha Vijana wengine zaidi wanapata Ajira.Kuhusiana na zao la karafuu Rais Dkt, Mwinyi amesema bado Serikali inalithamini zao hilo kuwa zao kuu la kiuchumi Serikali ina dhamira ya Kuliimarisha zaidi ili kuliongezea thamani.
Rais Dkt, Mwinyi amewaomba Wananchi wa Pemba kumchagua tena yeye ili aendelee kuleta Maendeleo zaidi pamoja na Dkt, Samia Suluhu Hassan kwa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.