Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt, Hussein Ali Mwinyi amesema Mafanikio makubwa ya Maendeleo yaliopatikana katika Uongozi wa Awamu ya Nane yamechangiwa na kuwepo kwa Amani ,Mshikamano na Utulivu Nchini.Rais Dkt, Mwinyi ameyasema hayo alipokutana na jopo la Wahariri na Waandishi wa Habari Ikulu leo tarehe 2 Septenba 2025.   

Amesema kuwepo kwa Mambo hayo matatu kumeiwezesha Serikali kutekeleza miradi mikubwa ya Maendeleo kwa Ufanisi Mkubwa Rais Dkt, Mwinyi amebainisha eneo jengine muhimu liliochangia Mafanikio hayo ni pamoja na ukusanyaji mzuri wa Mapato na Matumizi a Fedha za Serikali katika Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo.Ameeleza kuwa kwa muda mrefu Zanzibar ilishindwa kupiga hatua za Maendeleo kwa Wananchi Kutokuwa. wamoja ,kukosekana kwa Amani na Utulivu wa Nchi.   

Rais Dkt Mwinyi amesema Serikali imekuwa na Uwezo mzuri wa Kukopa   na Kuendesha miradi mikubwa kutokana na Ukusanyaji mzuri wa Kodi za Serikali.Aidha amefahamisha kuwa hatua hiyo pia imeijengea Hadhi Zanzibar ya kuweza kukopa na Kukopesheka kwa kuwa na Utaratibu bora wa Kulipa Madeni yake na kuaminika na Nchi na Taasisi za kimataifa.

Rais Dkt, Mwinyi ameeleza kuwa Serikali imeweka Akaunti maalum kwa ajili ya kuweka fedha za kulipa Madeni Yaani( Debt Management Account ) ambayo imekuwa ikiweka Dolla Milioni 15 kila Mwezi sawa na Dolla Milioni 180 kwa Mwaka. 

Akizungumzia Mipango ya Serikali kwa Awamu ijayo endapo itapata ridhaa ya Wananchi katika Uchaguzi Ujao ni kumaliza Changamoto zilizobakia katika Sekta zote muhimu ikiwemo Sekta ya Maji, Afya ,Elimu na Miundombinu ya Barabara. 

Akizungumzia Upatikanaji wa Maji amesema Serikali inaendelea na Mchakato wa kutekeleza Miradi mikubwa ya maji katika Mikoa ya Kaskazini na Kusini Unguja pamoja na Mkoa wa Mjini Magahribi ambayo itamaliza tatizo hilo katika muda mfupi ujao.     

Rais Dkt, Mwinyi amefahamisha kuwa. Serikali imedhamiria Kuweka Mkazo katika kuwajengea Uwezo Wataalamu wa Ndani ili kuimarisha Utoaji wa Huduma kwa Wananchi sambamba na kuimarisha Vyuo vya Amali kwa ajili ya kuwapatia Taaluma na Ujuzi Vijana ili waweze kuajirika na kujiajiri wenyewe.

Akizungumzia Uchaguzi Mkuu ujao Rais Dkt, Mwinyi amewanasihi Viongozi wa Dini , Wanasiasa na Waandishi wa Habari kuhubiri Amani na Mshikamano kabla ya Uchaguzi ,wakati na baada ya Uchaguzi. 

Mkutano huo wa Wahariri na Waandishi wa Habari wa Vyombo mbalimbali umefanyika baada ya Wahariri hao kutembelea Miradi Mikubwa ya Maendeleo iliotekelezwa na Serikali katika sekta mbalimbali Unguja na Pemba.