Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, leo tarehe 09 Septemba 2026 ameshiriki katika Hitma ya kumuombea Marehemu Hafidh Ameir Hassan, aliyekuwa Mwenza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Hitma hiyo imefanyika katika
Masjid Ikhtiswam Kizimkazi Mkunguni, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar, na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Serikali kutoka ndani na nje ya nchi, Viongozi wa Dini, familia, ndugu, jamaa , wasanii pamoja na wananchi kutoka makundi mbalimbali walioshiriki katika dua ya kumuombea Marehemu Hafidh Ameir Hassan.