Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amekutana na uongozi wa Benki ya Ecobank, ukiongozwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kitengo cha Wateja wa Biashara na Uwekezaji kutoka makao makuu ya benki hiyo nchini Togo, Bw. Michael Larbie, aliyefuatana na Afisa Mtendaji Mkuu wa Ecobank Tanzania, Ndugu Charles Asiedu, leo tarehe 15 Aprili 2026, Ikulu Zanzibar.
Katika mazungumzo hayo, Rais Dkt. Mwinyi ameishukuru Ecobank kwa kuendeleza ushirikiano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na kuunga mkono juhudi za maendeleo ya kiuchumi. Aidha, Rais Dkt. Mwinyi ameihakikishia benki hiyo ushirikiano endelevu, huku akibainisha fursa mbalimbali za uwekezaji, ikiwemo bandari, miundombinu ya barabara na uchumi wa buluu.
Kwa upande wake, Bw. Michael Larbie amesema Ecobank itaendelea kushirikiana na Zanzibar na kuimarisha ushirikiano wa kifedha na kibiashara barani Afrika kupitia mpango wake wa Pan African Partnership.
.jpeg)