Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amewasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Hamad, Jijini Doha, Qatar, tarehe 07 Oktoba 2026, kwa ziara ya kikazi inayolenga kuimarisha uhusiano na ushirikiano wa kiuchumi kati ya Zanzibar na Qatar, pamoja na kufungua fursa mpya za uwekezaji na maendeleo kwa Zanzibar.

Akiwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Hamad, Rais Dkt. Mwinyi amepokelewa na Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Qatar, Mhe. Habibu Awesi Mohamed.

Ziara hiyo ni sehemu ya juhudi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuimarisha diplomasia ya kiuchumi, kuvutia uwekezaji na kukuza ushirikiano wa kimkakati kwa manufaa ya wananchi wa Zanzibar.