Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amejumuika na mamia ya wananchi katika mazishi ya marehemu Sheikh Omar Bin Ali Qullaten, aliyefariki dunia jana akiwa anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Lumumba, Mkoa wa Mjini Magharibi.
Alhaj Dkt. Mwinyi ameshiriki pamoja na waumini wa dini ya Kiislamu katika Sala ya kumsalia marehemu, iliyofanyika katika Msikiti wa Gofu, Mkunazini, mnamo tarehe 21 Septemba 2025.
Katika tukio hilo, Rais Mwinyi aliungana na familia, ndugu, jamaa na waumini mbalimbali kuomboleza msiba huo na kumuombea marehemu Sheikh Omar Bin Ali Qullaten apumzishwe mahali pema peponi.