Rais wa na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt, Hussein Ali Mwinyi amejumuika na Waumini wa dini ya Kiislam katika Dua ya Kumuombea Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Mpendae Marehemu Salim Turky.Dua hiyo imefanyika leo tarehe 20 Julai 2025 Nyumbani kwa Marehemu Turky Mpendae ,Wilaya ya Mjini ,Mkoa wa Mjini Magharibi.     

Akitoa salamu zake Rais Dkt, Mwinyi ametoa wito kwa Watoto wema kuendelea kuwaombea dua Wazee wao waliotangulia Mbele ya haki na kuwahimiza kuendelea na Mwenendo huo mzuri.Alhaj Dkt, Mwinyi amewakumbusha Wananchi Umuhimu wa Kuiombea Nchi Amani ili iendelee kupiga hatua za Maendeleo.   

Amefahamisha kuwa Amani iliodumu kwa miaka mitano inapaswa Kudumishwa kwani kumekuwa na faida kubwa na Amani na Utulivu wa nchi kwani bila ya Amani hakuna maendeleo yatayopatikana kwenye Vurugu.Amesema kwa kipindi kirefu nchi ilikosa masikilizano na kuingia katika vurugu jambo lisilopaswa kujirudia. 

Rais Dkt, Mwinyi amebainisha kuwa kumekuwa na viashiria vya Uvunjifu wa Amani kutokana na kauli za baadhi ya Watu wanaotengeneza Mazingira ya kuirejesha Nchi katika Vurugu hasa wakati huu ikielekea katika Uchaguzi.Marehemu Salim Turky ametimiza Miaka Mitano tangu alipotangulia Mbele ya haki.