Katika mkutano huo uliofanyika Ikulu mjini Zanzibar ambapo pia, Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Idd alihudhuria, Wizara hiyo ya Afya ilieleza kuwa imeamua kuweka mikakati madhubuti katika kuhakikisha tatizo hilo linapatiwa suluhisho.
Mapema Waziri wa Wizara ya Afya, Mhe. Juma Duni Haji alieleza jinsi mikutano hiyo kati ya Wizara na Rais ilivyosaidia katika kupanga mipango mbali mbali ya Wizara na kumuhakikishia Rais kuwa watendaji wake wameweza kujifunza vyema kutokana na mikutano hiyo.
Uongozi huo chini ya Waziri wake Mhe. Juma Duni, ulieleza kuwa mbali ya juhudi hizo pia, imo katika mikakati ya kuhakikisha vifo akina mama na watoto watoto wachanga navyo vinapungua.