Aidha, Mama Mwanamwema Shein naye aliungana pamoja na akina mama wenzake wa kijiji hicho cha Mkanyageni katika futari hiyo ya pamoja.Wananchi hao waliyasema hayo wakati wakitoa neno la shukurani katika futari maalum walioandaliwa na Alhaj Dk. Shein hapo kijijini kwao Mkanyageni ikiwa ni utamaduni aliouweka wa kufutari nao pamoja kila ufikapo mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Akitoa neno hilo la shukurani kwa niaba ya wananchi wa Mkanyageni, Maalim Abdalla Yussuf alisema kuwa katika uongozi wa Alhaj Dk. Shein wananchi wameshuhudia mshikamano mkubwa sambamba na kuwepo kwa amani na utulivu ambavyo ndio dira ya maendeleo.

Maalim Abdalla alisema kuwa mbali ya shukurani kwa futari hiyo aliyowaandalia pia, wananchi wa Mkanyageni wanatoa shukurani za pekee kwa Alhaj Dk. Shein kwa kuifanyia mema Zanzibar.Mara baada ya futari hiyo kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein, Mkuu wa Wilaya ya Mkoani, Hemed Suleiman Abdalla alitoa shukurani kwa wananchi wote waliohudhuria katika hafla hiyo.

Alhaj Dk. Shein alieleza haja ya kuendeleza ushirikiano na mshikamano uliopo miongoni mwa wananchi wa Zanzibar sambamba na kuendelea kuishi kwa amani na utulivu.