RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amesema kuanzia mwezi Julai mwaka 2019, Zanzibar haitakuwa tena na tatizo la uhaba wa dawa kwa magonjwa yote yanayowakabilia wananchi wake.Alisema hilo linawezekana, kutokana na uchumi wa Zanzibar kuimarika hatua kwa hatua, hivyo wananchi wa Zanzibar wataondoka na shida walionayo hivi sasa, kwa uhaba wa dawa uliopo kwenye vituo vya afya pamoja na hospitali kadhaa.Dk. Shein alieleza hayo leo, huko katika uwanja mpira skuli ya Michenzani mara baada ya kukifungua kituo kipya cha afya cha Michenzani wilaya ya Mkoani, ikiwa ni shamra shamra za miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Alisema serikali inapotoa ahadi zake kwa wananchi huzitekeleza kwa wakati, hivyo nalo tatizo la kuondoa ubaha wa dawa kwa mujibu wa magonjwa yaliopo Zanzibar, linatarajiwa kuondoka kuanzia mwezi wa saba mwaka 2019.Dk. Shein alieleza kuwa, zipo ahadi kadhaa amezitoa kwa wananchi ikiwa ni pamoja na kuipandisha hadhi hospital ya Abdalla Mzee na kuwa ya Mkoa sambamba na kuingiza vifaa vya kisasa jamboa mbalo limeshakamilika.Alieleza kuwa, jengine ambalo ameliahidi na kulitekeleza ni kufuta michango ya elimu ngazi za msingi na sekondari, hivyo na hilo la ununuzi wa dawa zote linawezekana mara moja.