YALIYOMO ORODHA YA VIAMBATANISHO ...................................................….iv 

VIFUPISHO VYA MANENO .............................................................…vi 

UTANGULIZI .........................................................................................1 

MAPITIO YA UTEKELEZAJI WA PROGRAMU ZA AFISI YARAIS – IKULU KWA MWAKA WA FEDHA 2025/2026. ..............................................7 UTEKELEZAJI WA PROGRAMU ZA AFISI YA RAIS – IKULU (FUNGU A01). ....................................................................................7 i. Programu Kuu ya Kusimamia na Kuratibu Shughuli na Huduma za Mheshimiwa Rais na Kuimarisha Mawasiliano Ikulu. ........8 ii. Programu Kuu ya Kuratibu Ushirikiano wa Kikanda, Kimataifa na Wazanzibari Wanaoishi Nje ya Nchi. .............11 iii. Programu Kuu ya Utawala na Uendeshaji wa Afisi ya Rais – Ikulu. ...............................................................................14 UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MIRADI YA MAENDELEO .............17 MAPITIO YA UTEKELEZAJI WA OFISI YA BARAZA LA MAPINDUZI (FUNGU A02) KWA MWAKA WA FEDHA 2025/2026. .....................18 i. Programu Kuu ya Usimamizi wa Majukumu ya Kikatiba na Kisheria ya BLM. ......................................................................19 ii. Programu Kuu ya Utumishi na Uendeshaji wa Ofisi ya Baraza la Mapinduzi .............................................................20 MAPITIO YA UTEKELEZAJI WA PROGRAMU ZA TAASISI YA AFISI YA RAIS YA UFUATILIAJI NA USIMAMIZI WA UTENDAJI SERIKALINI ZANZIBAR (FUNGU A09) KWA MWAKA WA FEDHA 2025/2026. ……………………….....20 UTEKELEZAJI WA PROGRAMU ZA TAASISI YA ZPDB (FUNGU A09) .........21 i. Programu Kuu ya Usimamizi na Uratibu wa Huduma za Serikali .......................................................................................21 ii. Programu Kuu ya Mipango ya Miradi ya Kipaumbele na Uendeshaji. ............................................................................23 UTEKELEZAJI WA MRADI WA MAENDELEO KWA FUNGU A09 ……………......24 MAPITIO YA UTEKELEZAJI WA PROGRAMU ZA TAASISI YA NYARAKA NA KUMBUKUMBU ZANZIBAR (FUNGU A10) KWA MWAKA WA FEDHA 2025/2026. ....................................25 HOTUBA YA BAJETI WAZIRI WA NCHI AFISI YA RAIS -IKULU 2026/2027 ii i. Programu Kuu ya Usimamizi wa Nyaraka na Kumbukumbu kwa matumizi ya Serikali na Umma. ............25 ii. Programu Kuu ya Utawala na Uendeshaji wa Taasisi ya Nyaraka na Kumbukumbu. ..............................................27 MWELEKEO WA BAJETI YA AFISI YA RAIS – IKULU KWA MWAKA WA FEDHA 2026/2027 ......................................................................27. PROGRAMU KUU NA NDOGO NA MAKISIO YA FEDHA ZINAZOHITAJIKA KWA MWAKA WA FEDHA 2026/2027 ...............29 PROGRAMU KUU NA NDOGO ZA AFISI YA RAIS – IKULU (FUNGU 001) .................................................................................................30 i. Programu Kuu ya Usimamizi wa Shughuli za Mheshimiwa Rais na Uimarishaji wa Mawasiliano. ...................................30 ii. Programu Kuu ya Ushirikiano wa Kikanda, Kimataifa na Uratibu wa Wazanzibari Wanaoishi Nje ya Nchi. ................31 iii. Programu Kuu ya Utawala na Uendeshaji. ...........................32 MIRADI YA MAENDELEO ITAKAYOTEKELEZWA NA AFISI YA RAIS – IKULU KWA MWAKA WA FEDHA 2026/2027 ..................................33 PROGRAMU KUU NA NDOGO ZA OFISI YA BARAZA LA MAPINDUZI (FUNGU 040). ...................................................................................34 i. Programu Kuu ya Usimamizi wa Majukumu ya Kikatiba na Kisheria ya BLM. ................................................................34 ii. Programu Kuu ya Utumishi na Uendeshaji wa Ofisi ya Rais Baraza la Mapinduzi. ..............................................................35 PROGRAMU KUU NA NDOGO ZA TAASISI YA NYARAKA NA KUMBUKUMBU (FUNGU 057) ..........................................................36 i. Programu Kuu ya Usimamizi wa Nyaraka na Kumbukumbu kwa Matumizi ya Serikali na Umma. .....................................36 ii. Programu Kuu ya Utawala na Uendeshaji .........................37 PROGRAMU KUU NA NDOGO ZA TAASISI YA AFISI YA RAIS YA UFUATILIAJI NA USIMAMIZI WA UTENDAJI SERIKALINI (FUNGU 058) …….....38 i. Programu Kuu ya Usimamizi na Uratibu wa Miradi ya Serikali. ..................................................................................................38 HOTUBA YA BAJETI WAZIRI WA NCHI AFISI YA RAIS -IKULU 2026/2027 iii ii. Programu Kuu ya Mipango ya Miradi ya Kipaumbele na Uendeshaji. ..............................................................................39 MAOMBI YA FEDHA YA KAZI ZILIZOPANGWA KUTEKELEZWA KWA MWAKA WA FEDHA 2026/2027. .....................................................40 HITIMISHO ........................................................................................40 HOTUBA YA BAJETI WAZIRI WA NCHI AFISI YA RAIS -IKULU 2026/2027 iv ORODHA YA VIAMBATANISHO KIAMBATANISHO NAMBARI. 01. MUHTASARI WA MATUMIZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA MIEZI 9 (JULAI – MACHI) KWA MWAKA 2025 – 2026 KWA AFISI YA RAIS – IKULU (FUNGU 001) ..44 KIAMBATANISHO NAMBARI. 02. MUHTASARI WA MATUMIZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA MIEZI 9 (JULAI – MACHI) KWA MWAKA 2025 – 2026 KWA OFISI YA BARAZA LA MAPINDUZI (FUNGU 040) ....................................................................................47 KIAMBATANISHO NAMBARI. 03. MUHTASARI WA MATUMIZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA MIEZI 9 (JULAI – MACHI) KWA MWAKA 2025 – 2026 KWA TAASISI YA AFISI YA RAIS YA UFUATILIAJI NA USIMAMIZI WA UTENDAJI SERIKALINI (FUNGU 058) ...............48 KIAMBATANISHO NAMBARI. 04. MUHTASARI WA MATUMIZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA MIEZI 9 (JULAI - MACHI) KWA 2025 – 2026 KWA TAASISI YA NYARAKA NA KUMBUKUMBU (FUNGU 057) ....................................................................................49 KIAMBATANISHO NAMBARI. 05. ORODHA YA ZIARA ZA UKAGUZI WA MIRADI YA MAENDELEO. ........................................50 KIAMBATANISHO NAMBARI. 06. ORODHA YA ZIARA ZA UZINDUZI WA MIRADI YA MAENDELEO. ........................................51 KIAMBATANISHO NAMBARI. 07. ORODHA YA MIKUTANO YA KIKANDA NA KIMATAIFA AMBAYO RAIS WA ZANZIBAR AMESHIRIKI......................53 KIAMBATANISHO NAMBARI. 08. ORODHA YA VIKAO VYA MHESHIMIWA RAIS WIZARA ZA KISEKTA ZA SERIKALI ...................54 KIAMBATANISHO NAMBARI. 09. ORODHA YA MABALOZI NA WAGENI MASHUHURI WA NCHI ZA NJE WALIOMTEMBELEA MHESHIMIWA RAIS....................................................56 KIAMBATANISHO NAMBARI. 10. ORODHA YA IDADI YA SHEHIA ZILZOTEMBELEWA NA WANANCHI WALIOFIKIWA KATIKA MAFUNZO YA SNR..................................................... 58 KIAMBATANISHO NAMBARI. 11. USHIRIKI WA IDARA KATIKA MIKUTANO NA VIKAO ZA JUMUIYA ZA KIKANDA NA KIMATAIFA………………60 KIAMBATANISHO NAMBARI. 12. ORODHA YA MIKUTANO NA VIKAO YA URATIBU WA SHUGHULI ZA DIASPORA ZANZBAR. ......63 KIAMBATANISHO NAMBARI.13. ORODHA YA WATUMISHI WALIOPATIWA MAFUNZO. ............................................................. 64 v HOTUBA YA BAJETI WAZIRI WA NCHI AFISI YA RAIS -IKULU 2026/2027 VIFUPISHO VYA MANENO AfCFTA BLM CAN CCM EAC ECDP GSO ITV IORA NTBs PAC RAMIS SADC SNR TADIO TBC TOKTEN UAE UNDP UNFPA ZASO ZBC ZCTV ZNCC ZPDB Eneo huru la Biashara Barani Afrika Baraza la Mapinduzi Climate Action Network Tanzania Chama cha Mapinduzi Jumuiya ya Afrika Mashariki Early Childhood Development Programme Afisi ya Usalama wa Serikali Independent Television Indian Ocean Rim Association Non-Tariff Barriers Kamati ya Bajeti, na Kamati ya Kudumu ya Kudhibiti Hesabu za Serikali Mfumo wa kielektroniki wa uhifadhi na matumizi ya nyaraka na kumbumbuku Jumiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika Sema na Rais Mwinyi Jumuiya ya Watanzania wanaoishi nchini Oman Shirika la Utangazaji la Tanzania Transfer of knowlegde through expartriete Nationals Umoja wa Falme za Kiarabu United Nations Development Programme United Nations Population Fund Zanzibar Association of Sports Officers Shirika la Utangazaji la Zanzibar Zanzibar Cable Television Zanzibar National Chamber of Commerce Taasisi ya Afisi ya Rais ya Ufuatiliaji na Usimamizi wa Utendaji Serikalini Zanzibar. vi HOTUBA YA BAJETI WAZIRI WA NCHI AFISI YA RAIS -IKULU 2026/2027 UTANGULIZI 1. 2. 3. 4. Mheshimiwa Spika, Naomba kutoa hoja kwamba Baraza lako lipokee na kujadili Taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya Afisi ya Rais - Ikulu na Taasisi zake kwa Mwaka 2025/2026 na kupitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Afisi ya Rais - Ikulu (Fungu A01), Baraza la Mapinduzi (Fungu A02), Taasisi ya Afisi ya Rais ya Ufuatiliaji na Usimamizi wa utendaji Serikalini (Fungu A09), na Taasisi ya Nyaraka na Kumbukumbu (Fungu A10) kwa mwaka 2025/2026. Mheshimiwa Spika, Awali ya yote namshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa kutujalia uzima, siha njema, amani na utulivu vinavyotuwezesha kuendelea kutekeleza majukumu yetu yanayochangia kuleta maendeleo na kujenga ustawi wa Taifa. Pia, tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutuwezesha kukutana katika kipindi hiki cha Mkutano wa 03 wa Baraza la 11 kwa ajili ya kupokea utekelezaji wa Afisi ya Rais - Ikulu pamoja na kutafakari mipango ijayo katika kufikia malengo ya Nchi. Mheshimiwa Spika, Nchi yetu imetekeleza jukumu lake la kikatiba kwa kufanikisha Uchaguzi Mkuu uliofanyika mwezi Oktoba, 2025. Napenda kuwapongeza wananchi wote wa Zanzibar kwa kujitokeza kwa wingi kushiriki katika zoezi hilo muhimu la kidemokrasia, wakitumia haki yao ya msingi kwa amani na utulivu. Vilevile, napenda kuvipongeza vyama vyote vya siasa vilivyoshiriki katika Uchaguzi Mkuu, jambo linaloonesha kuimarika kwa misingi ya demokrasia nchini na ukomavu wa kisiasa miongoni mwa Watanzania. Mheshimiwa Spika, Kipekee napenda kutumia fursa hii kumshukuru Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, kwa imani yake kwangu na kuendelea kunipa dhamana ya kusimamia Afisi ya Rais - Ikulu, yenye jukumu kubwa la kusimamia na kuratibu utekelezaji wa sera na mipango ya Serikali, kuhakikisha nidhamu na utendaji bora wa watumishi wa umma na kukuza maendeleo endelevu ya kijamii, kiuchumi 1 HOTUBA YA BAJETI WAZIRI WA NCHI AFISI YA RAIS -IKULU 2026/2027 na kiutawala kwa wananchi na hatimae kuwa na Serikali yenye ufanisi na uwajibikaji kwa ustawi wa Taifa. 5. 6. 7. 8. Mheshimiwa Spika, Kwa heshima na adhama ya kipekee, napenda kutoa pongezi zangu za dhati kwa Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, kufuatia ushindi wa kishindo alioupata katika Uchaguzi Mkuu wa Vyama Vingi uliofanyika tarehe 29 Oktoba 2025. Ushindi huu ni kielelezo cha imani kubwa ya wananchi kwake, pamoja na uimara wa mikakati ya kisiasa iliyosimamiwa kwa umakini na maono ya muda mrefu. Mheshimiwa Spika, Kampeni za Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi zilijengwa juu ya msingi unaogusa uhalisia wa maisha ya wananchi, kuimarisha umoja wa kitaifa, kuchochea mageuzi ya kiuchumi na kudumisha misingi ya utawala bora. Ujumbe huu uliwasilishwa kwa utulivu, umakini na mwelekeo ulioeleweka kwa urahisi, hali iliyochangia kuimarisha uungwaji mkono kutoka kwa sekta mbalimbali za jamii. Mheshimiwa Spika, Katika kipindi chote cha kampeni, Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi aliendelea kujijengea taswira ya kuwa kiongozi makini, mwenye dira iliyo wazi na anayethamini maoni ya wananchi. Uwezo wake wa kusikiliza, kuelewa na kujibu changamoto za wananchi kwa vitendo uliimarisha zaidi uhusiano wa kuaminiana kati ya uongozi na jamii. Mheshimiwa Spika, Ushindi wake katika uchaguzi huo na hatimaye kuapishwa kwake rasmi tarehe 02 Novemba 2025, ni matokeo ya mchakato uliotekelezwa kwa nidhamu na ufanisi, ukihusisha mikakati madhubuti ya kisiasa, mawasiliano yenye ushawishi chanya, pamoja na mshikamano wa dhati kati ya chama na wananchi. Kwa ujumla, kampeni za Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi zilionesha kiwango cha juu cha ubora wa kisiasa na kimkakati. Ziliweka msingi imara wa ushindi huo na kuendelea kipindi cha pili cha awamu ya uongozi wake unaolenga kuharakisha maendeleo 2 HOTUBA YA BAJETI WAZIRI WA NCHI AFISI YA RAIS -IKULU 2026/2027 endelevu ya Zanzibar, kwa kuzingatia ustawi wa wananchi na mustakabali wa taifa kwa ujumla. 9. Mheshimiwa Spika, Natoa wito kwa wananchi na wadau wote kuendelea kushirikiana na Serikali katika kuimarisha juhudi za maendeleo ya taifa letu. Aidha, ninawakumbusha viongozi wote waliochaguliwa kuendelea kuweka mbele maslahi ya taifa katika utekelezaji wa majukumu yao, kwa kuwatumikia wananchi kwa uadilifu, uwazi na kujituma katika kila nafasi waliyopewa. 10. Mheshimiwa Spika, Mwaka mmoja ni kipindi kirefu katika maisha ya binadamu na mara nyingi huambatana na matukio na changamoto za maisha. Napenda kuwapa pole wananchi wote walioathiriwa na majanga yaliyotokea katika kipindi cha harakati zao za kujitafutia kipato na maisha. 11. Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea kuwa karibu na wananchi hao na itaendelea kushirikiana nao katika kukabiliana na changamoto hizo, kwa lengo la kuhakikisha wanapata msaada unaostahiki na kurejesha hali ya ustawi katika maisha yao. 12. Mheshimiwa Spika, Naomba kuliahidi Baraza lako Tukufu na wananchi wote kuwa nitaendelea kutekeleza majukumu yangu kwa uadilifu, bidii na weledi mkubwa, ili kuendeleza mafanikio yaliyofikiwa na kuhakikisha kwamba Bajeti hii inasimamiwa kwa ufanisi na kutekelezwa ipasavyo. Hakika, mafanikio makuu yaliyopatikana Zanzibar yametokana na maono ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi, katika kuwaletea Wazanzibari maendeleo endelevu. Tunajivunia na kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujalia kiongozi mwenye maono chanya kwa mustakabali wa Taifa letu. Naomba tuendelee kumuombea Mwenyezi Mungu amjalie afya njema, hekima, busara, na ustahimilivu katika kuliongoza Taifa letu. 3 HOTUBA YA BAJETI WAZIRI WA NCHI AFISI YA RAIS -IKULU 2026/2027 13. Mheshimiwa Spika, Nalikumbusha Baraza lako Tukufu kuwa Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ameweka wazi mwelekeo mpya wa Serikali katika kipindi chake cha pili, ukiangazia mageuzi ya kiuchumi na ustawi wa wananchi. Katika hotuba yake ya uzinduzi wa Baraza la kumi na moja la Wawakilishi tarehe 10 Novemba 2025, Mheshimiwa Rais alisisitiza kuwa Serikali itajikita katika kukuza ukuaji wa uchumi kwa kutumia nguvu za uzalishaji, kuongeza uwekezaji, na kuimarisha ushiriki wa sekta binafsi katika biashara na viwanda. 14. Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Rais Mwinyi pia alibainisha umuhimu wa kuimarisha utendaji wa sekta zinazochangia ukuaji wa uchumi, kuimarisha mazingira ya kupata mtaji, na kuendeleza fursa za uwekezaji zinazovutia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi. Mwelekeo huu mpya unalenga kuhakikisha maendeleo yanayojumuisha kila kona ya jamii; wakulima, wafanyabiashara wadogo na wakubwa, na vijana katika masuala ya ajira na ubunifu. 15. Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Rais amesisitiza usalama, amani, umoja wa kitaifa, na nidhamu ya kitaalamu kama misingi ya utekelezaji wa sera za uchumi na maendeleo endelevu katika kipindi cha miaka mitano ya uongozi wake. Serikali inalenga kujenga uchumi imara, wa kisasa, na wenye mshikamano, utakaowawezesha Wazanzibari kushindana vyema katika mazingira ya kimataifa ya kibiashara na kupata faida za moja kwa moja. 16. Mheshimiwa Spika, Napenda kutoa shukrani zangu za dhati na pongezi kwa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa uongozi wake madhubuti na wa kimkakati. Ameongoza jitihada za kukuza uchumi na kuimarisha maisha ya Watanzania, akiwahusisha wakulima, wafanyabiashara, na vijana katika maendeleo. Uongozi wake umeimarisha mazingira ya uwekezaji, kuimarisha miundombinu, na kuendeleza mshikamano wa kitaifa. Aidha, juhudi za Serikali zimepanua fursa za mikopo 4 HOTUBA YA BAJETI WAZIRI WA NCHI AFISI YA RAIS -IKULU 2026/2027 kwa wakulima, wavuvi, na wafugaji, kuongeza uzalishaji na kukuza uchumi wa kipato kwa wananchi. Mwelekeo huu unaonesha dhamira ya kujenga uchumi imara, wa kisasa, na unaotoa faida kwa kila mwananchi. 17. Mheshimiwa Spika, Kwa moyo wa dhati napenda kumshukuru Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdulla, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, kwa juhudi zake kubwa katika kuhakikisha Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inatekeleza majukumu yake kwa umakini. Ushirikiano wake na Mheshimiwa Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi umeimarisha ufanisi wa Serikali katika kutekeleza miradi ya maendeleo na kutoa huduma bora kwa wananchi. 18. Mheshimiwa Spika, Naomba nikupongeze wewe binafsi pamoja na Naibu Spika kwa kuliongoza Baraza letu Tukufu kwa umahiri mkubwa uliodhihirika katika kufikia maamuzi yenye manufaa kwa ustawi wa wananchi, hakika mmesimama imara kuongoza Muhimili huu muhimu kufanya maamuzi yenye tija kwa maendeleo ya Taifa na Mwenyezi Mungu aendelee kuwatia nguvu zaidi. Niwapongeze pia Wenyeviti wa Baraza kwa kukusaidia wewe kuongoza vyema vikao vya Baraza letu, ni dhahiri kuwa muhimili huu umetoa mchango mkubwa kwenye maamuzi ya nchi yetu. 19. Mheshimiwa Spika, Nichukue nafasi hii pia kuwapongeza Mawaziri wenzangu wote wa Serikali ya Awamu ya Nane kwa kuendelea kupewa dhamana ya kuwatumikia Wazanzibari na kwa kusimamia utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025/2030 na Dira ya Maendeleo ya Zanzibar ya mwaka 2050. 20. Mheshimiwa Spika, Nikiwa miongoni mwa watekelezaji wa Ilani ya CCM nichukue fursa hii kuwapongeza viongozi wote walioteuliwa kushika nafasi za kumsaidia Mwenyekiti kusimamia utekelezaji wa Ilani ya CCM. Tuendelee kushirikiana kutekeleza Ilani na miongozo mingine ya kitaifa ili kujenga Taifa letu. 5 HOTUBA YA BAJETI WAZIRI WA NCHI AFISI YA RAIS -IKULU 2026/2027 21. Mheshimiwa Spika, Napenda pia kutoa shukrani zangu za dhati kwa Balozi Mhandisi Zena Ahmed Said, aliyekuwa Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, kwa mchango wake mkubwa katika kuimarisha utendaji wa Serikali na kuhakikisha malengo yanafikiwa kwa ufanisi. Uongozi wake mahiri katika kusimamia watendaji wa Serikali umeacha alama muhimu ya mafanikio tunayojivunia leo. Aidha, tunampongeza kwa kuteuliwa kuwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Saudi Arabia na tunamtakia kila la kheri katika kuendelea kulitumikia Taifa katika nafasi hiyo mpya. 22. Mheshimiwa Spika, Vile vile, nawashukuru kwa dhati Kamati za Kudumu za Baraza la Wawakilishi, hususan Kamati ya Kusimamia Afisi za Viongozi Wakuu wa Kitaifa chini ya Mwenyekiti wake Mheshimiwa Machano Othman Said, Mwakilishi wa Jimbo la Mfenesini na Makamu wake Mheshimiwa Azza Januari Joseph, Mwakilishi wa Kuteuliwa kupitia nafasi Maalum za Wanawake pamoja na wajumbe wa kamati kwa ushirikiano, maelekezo na ushauri mzuri wanaotupatia ambao umetuwezesha kufanikisha utendaji wa kazi zetu. Aidha, nazishukuru Kamati ya Bajeti na Kamati ya Kudumu ya Kudhibiti Hesabu za Serikali (PAC), Ushirikiano, busara na maelekezo yao yamekuwa nyenzo muhimu katika kuimarisha utendaji wa Serikali. 23. Mheshimiwa Spika, Nichukue fursa adhimu ya kumshukuru na kumpongeza Ndugu Raya Issa Mselem, Katibu wa Baraza la Wawakilishi kwa Utendaji wake bora na mashirikiano anayonipa yeye binafsi na watendaji wengine wote wa Baraza la Wawakilishi. 24. Mheshimiwa Spika, ni wajibu wa kila mmoja wetu kuendelea kuiunga mkono Serikali, kudumisha mshikamano wa kitaifa, na kushiriki kikamilifu katika juhudi za kujenga Zanzibar imara yenye maendeleo jumuishi kwa ustawi wa wananchi. Ushirikiano huu ni nguzo muhimu katika kuimarisha utekelezaji wa sera na mipango ya maendeleo na kuhakikisha kuwa 6 HOTUBA YA BAJETI WAZIRI WA NCHI AFISI YA RAIS -IKULU 2026/2027 rasilimali za taifa zinatumika kwa ufanisi na kwa manufaa ya wananchi wote. 25. Mheshimiwa Spika, Katika Mwaka wa Fedha 2025/2026 Afisi ya Rais - Ikulu iliwasilisha mbele ya Baraza lako Tukufu, Mpango na Bajeti ya Afisi na kuomba fedha ili kutekeleza majukumu yake. Ninayo heshima kusimama tena mbele ya Baraza lako Tukufu ili niweze kutoa taarifa ya utekelezaji wa Mpango ulioombewa fedha kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026 na kuwasilisha Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2026/2027. MAPITIO YA UTEKELEZAJI WA PROGRAMU ZA AFISI YA RAIS – IKULU KWA MWAKA WA FEDHA 2025/2026. 26. Mheshimiwa Spika, Afisi ya Rais - Ikulu, kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026 ilijipangia kutekeleza Programu Kuu tisa (09) zenye Programu ndogo kumi na tano (15). Kiambatanisho nambari 01, 02, 03 na 04 vina maelezo ya ziada kuhusu Programu Kuu na Programu Ndogo. UTEKELEZAJI WA PROGRAMU ZA AFISI YA RAIS – IKULU (FUNGUA01). 27. Mheshimiwa Spika, Fungu A01 limejumuisha Programu Kuu tatu na Programu Ndogo nane. Kwa kipindi cha Julai, 2025 hadi Machi 2026, fungu hili limetumia TZS. 7.94.Bilioni sawa na asilimia 51.87 ya makadirio ya TZS.15.30 Bilioni kwa kipindi cha tathmini na asilimia 39.52 ya makadirio ya kutumia TZS. 20.09 Bilioni kwa mwaka. Mchanganuo wa matumizi hayo ni kama ifuatavyo: a) Malipo ya Mishahara TZS. 5.06 Bilioni sawa na asilimia 98.78 ya makadirio ya TZS, 5.12 Bilioni kwa kipindi cha tathmini. b) Matumizi Mengineyo TZS. 1.51 Bilioni sawa na asilimia 43.34 ya makadirio ya TZS. 3.49 Bilioni kwa kipindi cha tathmini. 7 HOTUBA YA BAJETI WAZIRI WA NCHI AFISI YA RAIS -IKULU 2026/2027 c) Matumizi ya Mradi wa Maendeleo TZS.1.37 Bilioni sawa na asilimia 20.46 ya makadirio ya TZS. 6.70 Bilioni kwa kipindi cha tathmini. 28. Mheshimiwa Spika, Fedha hizo zimetumika kutekeleza programu kuu zifuatazo: i. Programu Kuu ya Kusimamia na Kuratibu Shughuli na Huduma za Mheshimiwa Rais na Kuimarisha Mawasiliano Ikulu. 29. Mheshimiwa Spika, Hadi kufikia Machi 2026, programu hii imetumia TZS. 3.88 Bilioni sawa na asilimia 85.67 ya makadirio ya TZS. 4.53 Bilioni kwa kipindi cha tathmini na asilimia 64.81 ya makadirio ya TZS. 5.99 Bilioni kwa mwaka. Programu kuu hii imejumuisha programu ndogo mbili zifuatazo: a) Programu ndogo ya Uratibu wa Huduma za Mheshimiwa Rais imetumia TZS. 3.39 Bilioni sawa na asilimia 91.60 ya makadirio ya kutumia TZS.3.70 Bilioni kwa kipindi cha tathmini; na b) Programu ndogo ya Kuimarisha Mawasiliano baina ya Serikali na Wananchi imetumia TZS. 492.89 Milioni sawa na asilimia 59.27 ya makadirio ya kutumia TZS. 831.63 Milioni kwa kipindi cha tathmini. 30. Mheshimiwa Spika, kupitia Programu hii, Afisi imetekeleza yafuatayo: i. Kutoa ushauri kwa Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi katika masuala ya siasa, uchumi, jamii, sheria, diplomasia, mawasiliano na habari, pamoja na uhusiano wa kikanda na kimataifa, na masuala mengine muhimu. ii. Kusimamia ratiba ya kila siku ya Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, kuhakikisha kwamba shughuli zake zinatekelezwa kwa mujibu wa mipango iliyowekwa na kwa ufanisi unaotarajiwa. 8 HOTUBA YA BAJETI WAZIRI WA NCHI AFISI YA RAIS -IKULU 2026/2027 iii. Ziara nane (08) za ukaguzi wa miradi ya maendeleo ndani ya visiwa vya Zanzibar zimefanyika. Ziara hizi zimehusu ukaguzi wa miradi katika sekta ya elimu, afya, michezo, maji, miundombinu na kilimo, kwa lengo la kuhakikisha utekelezaji wake unakidhi viwango vinavyotarajiwa, kutumia rasilimali kwa ufanisi na kutoa mapendekezo ya kuimarisha miradi hii ili kufanikisha maendeleo endelevu kwa wananchi. Kiambatanisho nambari 05 kina taarifa zaidi. iv. Kuratibu uzinduzi wa miradi kumi na nane (18) mikubwa, miradi ambayo ina faida za moja kwa moja kwa wananchi katika sekta ya elimu, afya, maji, nishati na miundombinu. Miradi hii inalenga kuimarisha huduma za jamii, kuongeza fursa za kiuchumi, na kuhakikisha maendeleo endelevu yanayogusa maisha ya kila siku ya wananchi. Kiambatanisho nambari 06 kina taarifa zaidi. v. Kuratibu ushiriki wa Mheshimiwa Rais katika mikutano minne (04) ya kikanda na kimataifa yenye lengo la kukuza ushirikiano wa kibiashara, uwekezaji na maendeleo ya kiuchumi. Mikutano hii imejumuisha Mkutano wa Mabaraza ya Habari Afrika, Mkutano wa Usajili Barani Afrika na Mkutano wa Uhakiki wa Rasimu ya Mkakati wa kuboresha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji. Ushiriki huu umehusisha mazungumzo na wadau mbalimbali, kutafuta fursa za uwekezaji, kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia na kushirikiana katika miradi ya maendeleo, ili kuhakikisha Zanzibar inapata faida za kiuchumi na kimaendeleo. Kiambatanisho nambari 07 kina taarifa zaidi. vi. Kuratibu na kuendesha vikao 22 vya kiserikali. Vikao hivi vilitumika kutoa maelekezo ya kiutendaji kwa wizara na taasisi 17 za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Kupitia vikao hivi, Mheshimiwa Rais amesisitiza uwajibikaji na nidhamu katika utekelezaji wa majukumu ya Serikali. Kiambatanisho nambari 08 kina taarifa zaidi. 9 HOTUBA YA BAJETI WAZIRI WA NCHI AFISI YA RAIS -IKULU 2026/2027 vii.Kuratibu na kufanikisha shughuli ya kutunuku Nishani ya Mapinduzi na Nishani ya Utumishi Uliotukuka kwa viongozi na wananchi 18 wenye sifa maalum, ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wao katika historia, maendeleo na ustawi wa Zanzibar. viii.Kuratibu hafla ya utiaji saini wa mikataba ya miradi mitatu mikubwa ya kimkakati iliyofanyika Ikulu Zanzibar, ikiwemo mradi wa Mfumo Jumuishi wa Usimamizi na Usajili wa Huduma za Ardhi, Mradi wa Usambazaji Maji Kusini Unguja na ujenzi wa Kituo cha Huduma za Saratani Binguni. Miradi hii inalenga kutatua changamoto za muda mrefu katika sekta za ardhi, maji na afya pamoja na kuimarisha upatikanaji wa huduma muhimu kwa wananchi. ix. Kuratibu na kutekeleza itifaki ya mikutano ya Mheshimiwa Rais na mabalozi na wajumbe kutoka nchi mbalimbali ikiwemo Marekani, Saudi Arabia, Ufaransa, Oman, Canada, India na Brazil, kwa lengo la kukuza ushirikiano wa kimkakati na kuvutia uwekezaji. Katika mikutano hii, majadiliano yamelenga sekta za kipaumbele zikiwemo miundombinu, utalii, afya, elimu, uchumi wa buluu na biashara. Majadiliano hayo yalisisitiza upatikanaji wa fursa za uwekezaji, misaada ya maendeleo na uhamishaji wa teknolojia. Aidha, mikutano hiyo imeimarisha uhusiano wa kidiplomasia, kuongeza imani ya washirika wa kimataifa na kufungua fursa mpya za maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa Zanzibar. Kiambatanisho nambari 09 kina taarifa zaidi. x. Kusimamia utayarishaji, urushaji na utangazaji wa shughuli za kila siku zinazotekelezwa na Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi kupitia vyombo vya habari vikiwemo ZBC TV na Redio, Channel Ten, ITV, TBC Taifa, ZCTV na Azam TV. 10 HOTUBA YA BAJETI WAZIRI WA NCHI AFISI YA RAIS -IKULU 2026/2027 xi. Kuimarisha mawasiliano kati ya Mheshimiwa Rais na wananchi kupitia mitandao ya kijamii iliyofikia maelfu ya watembeleaji “Followers” (Facebook yenye watembeleaji 114,063, Instagram 378,000 na Whatsapp 47,467). xii. Kupitia Mfumo wa Sema na Rais Mwinyi (SNR), Afisi imepokea malalamiko 5,266 kati ya hayo, malalamiko 4,593 sawa na asilimia 87.2 yamepatiwa ufumbuzi, na malalamiko 673 sawa na asilimia 12.8 yakiendelea kufuatiliwa kwa kushirikiana na taasisi husika ili kupatiwa ufumbuzi wa kudumu. xiii. Kuandaa na kurusha hewani vipindi 36 kupitia Shirika la Utangazaji Zanzibar kwa lengo la kuonesha ushuhuda wa utatuzi wa changamoto za wananchi zinazowasilishwa kupitia Mfumo wa Sema na Rais, jambo lililoshajihisha wananchi kutumia mfumo huo. xiv.Kutoa mafunzo ya matumizi ya Mfumo wa SNR kwa wananchi 2,518 kutoka shehia 44 za Unguja na Pemba. Kiambatanisho nambari 10 kina taarifa zaidi. ii. Programu Kuu ya Kuratibu Ushirikiano wa Kikanda, Kimataifa na Wazanzibari Wanaoishi Nje ya Nchi. 31. Mheshimiwa Spika, Hadi kufikia Machi 2026, programu hii imetumia TZS. 307.02 Milioni sawa na asilimia 47.81 ya makadirio ya TZS. 642.19 Milioni kwa kipindi cha tathmini na asilimia 37.22 ya makadirio ya TZS. 824.88 Milioni kwa mwaka. Programu kuu hii imejumuisha programu ndogo mbili zifuatazo: a) Programu ndogo ya Uratibu wa Shughuli za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kikanda na kimataifa imetumia TZS. 275.52 Milioni sawa na asilimia 53.59 ya makadirio ya kutumia TZS. 514.15 Milioni kwa kipindi cha tathmini; na b) Programu ndogo ya Uratibu Shughuli za Wazanzibari wanaoishi nje ya nchi imetumia TZS. 31.50 Milioni sawa na 11 HOTUBA YA BAJETI WAZIRI WA NCHI AFISI YA RAIS -IKULU 2026/2027 asilimia 24.60 ya makadirio ya kutumia TZS.128.04 Milioni kwa kipindi cha tathmini. 32. Mheshimiwa Spika, Kupitia Programu hii, Afisi imetekeleza yafuatayo: i. Kuratibu ushiriki wa Zanzibar katika Mikutano ya Jumuiya za Kikanda (EAC, SADC, AfCFTA, IORA) na ushirikiano wa Kimataifa kwa ajili ya utatuzi wa changamoto na upatikanaji wa fursa kwa Zanzibar. ii. Afisi imeshiriki Vikao na Mikutano 17 ya Jumuiya za Kikanda za EAC, SADC na AfCFTA ndani na nje ya nchi. Lengo la vikao na mikutano hiyo ni upatikanaji wa fursa na kuwajengea uwezo wadau katika kukuza sekta muhimu za Uchumi ikiwemo Uchumi wa buluu, uwekezaji, Biashara na Ujasiriamali Kiambatanisho nambari 11 kina taarifa zaidi. iii. Afisi imetoa mafunzo ya Vikwazo Visivyo vya Kodi (NTBs) kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa wataalamu 32 kutoka Kamati ya NTBs ya Zanzibar, Wafanya Biashara na watendaji kutoka Jumuiya ya Wafanya Biashara Zanzibar. Mafunzo hayo yalilenga kuimarisha uelewa kuhusu dhana na athari za Vikwazo Visivyo vya Kodi katika biashara na kujenga uwezo wa washiriki katika kutambua na kushughulikia vikwazo hivyo kwa ufanisi. iv. Kuratibu shughuli 128 za Itifaki ya Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pamoja na kuratibu safari saba za Viongozi Wakuu wastaafu nje ya nchi. v. Kushiriki mikutano mitano (5) inayohusiana na masuala ya Diaspora ikiwemo mikutano ya taarifa za wahamaji (Data Migration), ubidhaishwaji wa lugha ya Kiswahili pamoja na vikao vya mashirikiano baina ya Afisi na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Kiambatanisho nambari 12 kinataarifa zaidi. 12 HOTUBA YA BAJETI WAZIRI WA NCHI AFISI YA RAIS -IKULU 2026/2027 vi. Uzinduzi wa Mfumo rasmi wa Usajili wa Diaspora wa Zanzibar (mwezi Januari 2026), unaoiwezesha Serikali kupata takwimu halisi za Diaspora wa Zanzibar ikiwemo nchi wanazoishi, taaluma na ujuzi, biashara na uwekezaji kwa lengo la kushirikiana katika maswala ya Uchumi, fursa na maendeleo. Hadi kufikia mwezi Machi, 2026, Afisi imesajili Diaspora 1,360 kutoka mataifa mbali mbali duniani. Aidha, kwa kipindi hicho Disapora 423 Wameshapatiwa vitambulisho vyao (Wanaume 257 na Wanawake 166). vii. Afisi imeratibu maombi 17 ya vibali vya kazi na maombi 22 ya vibali vya ukaazi kwa Diaspora ambao wanahitaji kukaa nchini na kuendelea na shughuli zao za kiuchumi. viii. Afisi kwa kushirikiana na Jumuiya ya Diaspora Al Amana Foundation kutoka Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), imeratibu utoaji wa sadaka ya futari kwa familia zaidi ya 1200 yenye thamani TZS.100.00 Milioni na kuwalipia faini na fidia yenye thamani ya TZS. 18.4 Milioni kwa Wanafunzi 18 walioachiwa huru na kutoa msaada wa magodoro 170 kwa ajili ya Chuo cha Mafunzo. ix. Afisi kwa kushirikiana na Kamisheni ya Wakfu na Mali ya Amana Zanzibar na Chuo cha Mafunzo imeratibu mafunzo ya imani kwa Wanafunzi 18 wa Chuo cha Mafunzo walioachiwa huru. x. Afisi iliratibu na kushiriki katika zoezi la utoaji wa misaada ya kijamii kwa familia 600 yenye thamani ya zaidi ya TZS. 43.75 Milioni kisiwani Pemba. Misaada hiyo ilitolewa na Jumuiya ya Watanzania wanaoishi nchini Oman (TADIO), Al Wadood Charitable Group na Taasisi ya Diaspora Charity Organization za nchini Oman. xi. Afisi kwa kushirikiana na Afisi ya Mufti wa Zanzibar imeratibu uingizwaji wa kontena la sadaka liloletwa na Jumuiya ya Diaspora Ifraj Zanzibar Foundation iliyopo Umoja wa 13 HOTUBA YA BAJETI WAZIRI WA NCHI AFISI YA RAIS -IKULU 2026/2027 Falme za Kiarabu (UAE). Sadaka hio iliwanufaisha familia (668 - Unguja na 5,350 – Pemba) na yenye thamani ya TZS. 377.16 Milioni. xii. Afisi ilifanikiwa kukusanya TZS. 13.15 Milioni kutoka Diaspora wa Zanzibar Duniani kwa ajili ya utoaji wa Sadaka katika mwezi Mtukufu wa Ramadhan. Sadaka hio walipatiwa watoto 382 ikiwemo mayatima na wenye mahitaji maalum kwa Unguja na Pemba. xiii. Afisi imeratibu programu ya TOKTEN (Tranfer of Knowlegde Through Expatriate Nationals) kwa Wizara na Taasisi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Wataalam wawili (02) kutoka jamii ya Diaspora (Uingereza na Afrika Kusini) walibadilishana ujuzi na uzoefu kwa Wizara na Taasisi za Serikali katika masuala ya ubunifu, Akili Mnemba pamoja na usimamizi wa huduma za maji safi na salama kwa jamii. xiv. Afisi imefanya vikao viwili (02) vya majadiliano na Diaspora, vikao hivyo vilikutanisha wanadiaspora na taasisi husika zinazotoa huduma kwa Diaspora ambapo wanadiaspora walipata fursa ya kueleza changamoto zao na kutatuliwa. Lengo la vikao hivyo ni kuweka mfumo endelevu wa mawasiliano na kuimarisha uhusiano wa Diaspora na nchi yao ya asili. iii. Programu Kuu ya Utawala na Uendeshaji wa Afisi ya Rais – Ikulu. 33. Mheshimiwa Spika, Hadi kufikia Machi 2026, programu hii imetumia TZS. 3.75 Bilioni sawa na asilimia 37.00 ya makadirio ya TZS. 10.13 Bilioni Kwa kipindi cha tathmini na asilimia 28.24 ya makadirio ya TZS. 13.27 Bilioni kwa mwaka. Programu kuu hii imejumuisha programu ndogo nne zifuatazo: a) Programu ndogo ya Uratibu na Usimamizi wa Afisi ya Rais Ikulu imetumia TZS.1.31 Bilioni sawa na asilimia 76.92 ya makadirio ya kutumia TZS. 1.697 Bilioni kwa kipindi cha tathmini. 14 HOTUBA YA BAJETI WAZIRI WA NCHI AFISI YA RAIS -IKULU 2026/2027 b) Programu ndogo ya Uratibu wa shughuli za Mipango, Sera na Utafiti imetumia TZS.1.59 Bilioni sawa na asilimia 22.80 ya makadirio ya kutumia TZS. 6.98 Bilioni kwa kipindi cha tathmini. c) Programu ndogo ya Uratibu na Usimamizi wa Afisi ya Rais Ikulu Pemba imetumia TZS. 733.81 Milioni sawa na asilimia 64.68 ya makadirio ya kutumia TZS. 1.13 Bilioni kwa kipindi cha tathmini. d) Programu ndogo ya Usimamizi wa Usalama wa Serikali imetumia TZS. 117.00 Milioni sawa na asilimia 36.84 ya makadirio ya kutumia TZS. 317.61 Milioni kwa kipindi cha tathmini. 34. Mheshimiwa Spika, kupitia Programu hii, Afisi imetekeleza yafuatayo: i. Kuandaa Kanuni za Utoaji wa Tunzo (Nishani) 2025 chini ya Sheria ya mambo ya Rais. Nam. 3 ya mwaka 2020. ii. Kuratibu na kusimamia utoaji wa stahiki kwa watumishi kwa mujibu wa sheria na kanuni za utumishi wa umma kwa lengo la kuongeza hamasa katika utekelezaji wa majukumu ya kazi. iii. Kufanya ukaguzi wa kipindi cha robo ya nne ya Mwaka wa Fedha 2024/2025, sambamba na ukaguzi wa robo ya kwanza, ya pili na ya tatu ya Mwaka wa Fedha 2025/2026, kwa lengo la kutathmini utekelezaji wa shughuli, ufanisi wa matumizi ya rasilimali, pamoja na kuainisha na kushauri maeneo yanayohitaji kuimarishwa kwa kuzingatia viwango na miongozo ya ukaguzi wa ndani. iv. Kuwajengea uwezo watumishi 42 kwa kuwapatia mafunzo ya muda mrefu katika ngazi na fani zinazohitajika za elimu, pamoja na mafunzo ya muda mfupi ikiwemo Programu za kuwajengea ujuzi kazini na maandalizi ya kustaafu utumishi wa umma kwa lengo la kuimarisha 15 HOTUBA YA BAJETI WAZIRI WA NCHI AFISI YA RAIS -IKULU 2026/2027 utendaji kazi. Kiambatanisho nambari 13 kinataarifa zaidi. v. Kuhakiki mali za Afisi ya Rais - Ikulu kwa kuzitambua, kuziweka thamani stahiki na kuzisajili katika Mfumo wa Usimamizi wa Mali wa Serikali. vi. Kufanya tathmini ya utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Afisi kwa kipindi cha mwaka 2023/2024 hadi 2025/2026, kwa lengo la kupima kiwango cha utekelezaji wa malengo yaliyowekwa, kubaini mafanikio yaliyopatikana, changamoto zilizojitokeza, na kuainisha hatua stahiki za kuimarisha utendaji. vii. Kufanya tathmini ya utendaji wa Afisi ya Usalama wa Serikali pamoja na hali halisi ya usalama katika Ofisi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. viii. Kufanya upekuzi wa kiusalama wa awali na endelevu kwa watumishi 1,739. Hatua hii imeimarisha uadilifu na uaminifu miongoni mwa watumishi wa umma, hususan katika nafasi nyeti, na hivyo kupunguza kwa kiasi kikubwa vihatarishi vya kiusalama vinavyoweza kujitokeza. ix. Kufanya ukaguzi wa miundombinu na majengo ya Serikali kumi na moja (11), pamoja na mifumo ya TEHAMA katika taasisi tatu (3) za Serikali. Ukaguzi huu umewezesha kutathmini hali ya usalama wa nyaraka, taarifa, maeneo ya kazi na ufanisi wa mifumo ya utoaji huduma. x. Kutoa mafunzo maalum ya kiusalama kwa wateule 78. Mafunzo yalilenga kuongeza uelewa wao wa kiusalama, kuimarisha utendaji katika majukumu yao na kudumisha nidhamu. xi. Kutoa mafunzo maalumu ya kiusalama katika mifumo ya TEHAMA na vifaa vya kielektroniki kwa taasisi tatu (03) za Serikali, mafunzo yalilenga kuimarisha uelewa 16 HOTUBA YA BAJETI WAZIRI WA NCHI AFISI YA RAIS -IKULU 2026/2027 wa watumishi, utendaji wao na kuhakikisha usalama wa matumizi ya mifumo muhimu ya kiserikali. xii. Kutoa mafunzo kwa watumishi wa umma kwa taasisi 32. Mafunzo haya yalilenga kuimarisha uelewa wa watumishi juu dhana ya usalama serikalini. xiii. Kuimarisha mifumo ya ufuatiliaji na uratibu kwa waajiriwa wapya na wateule wa Rais. Shughuli hizi zinaweka msingi mzuri wa kudhibiti rasilimali watu na kuimarisha usalama, huku zikiwa na lengo la kuongeza ufanisi wa GSO katika kipindi kijacho. xiv. Kufuatilia ahadi za Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi katika miradi ya maendeleo kwa upande wa Pemba. Ahadi hizo zimejumuisha Miradi ya Maendeleo ya Ujenzi wa Barabara ya Ukutini – Mtangani, Finya – Kicha, Chuo cha Mwalimu Nyerere Tawi la Pemba, Dahalia ya Skuli ya Sekondari ya Kiwani na Fidel Castro. xv. Kutoa mafunzo ya Sera na Sheria ya Diaspora kwa masheha 32 wa Wilaya ya Chake Chake Pemba. Lengo la mafunzo hayo ni kujenga uelewa kwa masheha juu ya namna kufahamu fursa na huduma wanazopewa Diaspora na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. xvi. Kuandaa na kurusha vipindi vinne (4) vinavyoonesha uwajibikaji wa Serikali ya awamu ya nane kwa jamii kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii Pemba. UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MIRADI YA MAENDELEO 35. Mheshimiwa Spika, Kwa kipindi cha miezi tisa, Afisi ya Rais - Ikulu ilipangiwa TZS. 6.70 Bilioni kwa utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo. Miradi hiyo ni Mradi wa Uimarishaji wa majengo ya Ikulu, Mradi wa Uimarishaji Mawasiliano ya Mfumo wa Sema na Rais na Mradi wa Uimarishaji wa 17 HOTUBA YA BAJETI WAZIRI WA NCHI AFISI YA RAIS -IKULU 2026/2027 Mfumo wa Ulinzi na Usalama katika Majengo ya Ikulu na Makaazi ya Mheshimiwa Rais. Hadi kufikia Machi 2026, Afisi imeingiziwa TZS. 1.37 Bilioni sawa na asilimia 20.46. 36. Mheshimiwa Spika, Kupitia shughuli za miradi ya maendeleo, Afisi imetekeleza yafuatayo: i. Kufanya ukarabati wa majengo ya Ikulu Ndogo ya Dodoma na Ikulu Ndogo ya Laibon Dar es salaam ikiwemo uwekaji wa paving stone na curb stone mpya katika maeneo ya ndani ya Ikulu. ii. Kuimarisha mifumo ya ulinzi katika Ikulu Ndogo ya Pagali kwa kuweka kamera za uangalizi (CCTV), pamoja na uzio wa umeme, kwa lengo la kuongeza kiwango cha usalama na ulinzi wa eneo hilo. iii. Kuweka lifti katika Ikulu ya Mnazi Mmoja ili kuimarisha upatikanaji wa huduma na kurahisisha ufikiaji wa maeneo ya ofisi, hususan kwa wageni wanaofika kushiriki vikao na mikutano na Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, hatua inayochangia kuongeza ufanisi wa shughuli za kiutawala na hadhi ya mazingira ya kikazi. iv. Kununua vitendea kazi vinavyohitajika katika kutoa huduma kwa Uongozi, ikiwemo vifaa vya kisasa vya uendeshaji wa mikutano, mifumo ya sauti (PA system), vifaa vya TEHAMA, mifumo ya mawasiliano ya ndani, pamoja na vifaa maalum vya mapokezi na mikutano ya viongozi wakuu wa Serikali, kwa lengo la kuimarisha ufanisi, hadhi na weledi katika utekelezaji wa majukumu ya kiutawala