Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt, Hussein Ali Mwinyi amewanasihi Waumini wa Dini ya Kiislamu na Wananchi kwa Ujumla kuendelea kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa Neema ya Amani iliyopo Hapa nchini.
Alhaji Dkt, Mwinyi ameyasema hayo leo tarehe 19 Doisemba 2025 alipojumuika na Waumini wa Dini ya Kiislamu katika Ibada ya Sala ya Ijumaa iliyosaliwa Msikiti wa Miembeni, Mkoa wa Mjini Magharibi.
Ameeleza kuwa Kufanyika kwa Uchaguzi kwa Amani ni jambo la Kihistoria linalowapasa Wananchi kumshukuru Mungu na ni wajibu wa kila mmoja kushukuru na kuendelea kumuomba Mwenyezi Mungu aijalie Nchi Amani zaidi ili Serikali iweze kutekeleza mipango zaidi ya Maendeleo.
Alhaji Dkt, Mwinyi amempongeza Mfadhili alieyejitokeza kujenga Msikiti Mpya Mkubwa na wa kisasa katika Eneo hilo la Miembeni na kuwahimiza Waumini kumuombea dua ili kufanikisha Ujenzi huo .
Naye Katibu Mtendaji wa Afisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khalid Ali Mfaume amewahimiza Waumini wa Dini ya Kiislamu Kuutumia Vema muda wa Maisha yao hapa Duniani kwa Kutenda Mambo mema yatakayompendezesha Mwenye Mungu..
_770_513shar-50brig-20.jpeg)