Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt, Hussein Ali Mwinyi amevisisitiza Vyuo Vikuu hapa Nchini kuongeza kasi ya Kufanya Tafiti nyingi zaidi zitakazosaidia kutatua Changamoto zinazoikabili Jamii. Rais Dķt, Mwinyi ameyasema hayo leo tarehe 13 Disemba 2025 katika Maghafali ya 25 ya Chuo Kikuu cha Abdulrahman Al Sumait, Chukwani, Mkoa wa Mjini Magharibi.
Rais Dķt, Mwinyi ameeleza kuwa. Ni vyema tafiti zinazofanyika zikatumika kuleta Matokeo na Mchango wa Maendeleo ya Nchi na jamii badala ya kubakia bila ya kutumika. Amefahamisha kuwa tafiti nyingi zimebaki bila kutumika na kusambazwa. Kwa jamii na hatimaye kutosaidia kutoa mchango wa utatuzi wa changamoto za kijamii.
Dkt, Mwinyi amesema kutotumika kwa tafifti zinazofanyika katika Vyuo Vikuu kumekuwa kukivishushia hadhi Vyuo Vikuu ndani ya jamii na kutochangia maendeleo ya Nchi kama ilivyokusudiwa. Rais Dķt, Mwinyi amesema Serikali inathamini Mchango Mkubwa unaotolewa na Chuo Kikiuu cha Abdulrahman Ali Sumait wa kuendelea kuandaa Wataalamu wa fani mbali na kwamba itaendelea kuunga mkono juhudi hizo.
Amepongeza Mchango unaotolewa na Sekta binafsi kukuza Elimu na kuipongeza Taasisi ya Direct Aids ya Kuwait kwa Mchango mkubwa inayoendelea kuitoa kwa Chuo hicho na kukuza Sekta ya Elimu hapa Nchini pamoja na kuupongeza Uongozi wa Chuo kwa uamuzi wa kuanzisha kozi mpya Chuoni hapo ikiwemo kozi ya Shahada ya Uzamili katika Teknolojia ya Habari na Mawasiliano na kozi za muda mfupi kwa Watumishi wa Umma.
Aidha Rais Dķt, Mwinyi amepongeza hatua ya uimarishaji wa Miundombinu ya Chuo hicho ambapo Shilingi Bilioni 4 zimetumika kwa Ujenzi wa Jengo ,ununuzi wa Vifaa vya mafunzo ya ICT uliogharimu Shilingi Milioni 800 na ununuzi wa samani uliogharimu shilingi Milioni 600.
Kutokana na uwekezaji huo ametoa wito kwa Uongozi, wa Chuo hicho kutumia ipasavyo miundombinu iliowekwa kuongeza ufanisi na kukifanya chuo hicho kuwa kitovu cha ufundishaji wa fani ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Afika Mashariki.
Jumla ya Wahitiimu 679 wamehitimu mwaka 2025 na kutunukiwa Shahada ya kwanza(Bachelor Degree),Shahdaa ya Umahiri (Master’s Degrree) Stashahada na Astashada ambapo asilimia 64.5 ni Wanawake na asilimia 35.5 ni Wahitimu Wanaume.
Rais Dķt, Mwinyi ametoa Wito kwa Wahitimu hao Kuleta mabadiliko na maendeleo kwa nchi na jamii pamoja na kuishi kwa maadili na nidhamu na kuwa mfano ndani ya jamii kwa kutoa mchango wao kwa maendeleo ya nchi.
Akizungumza katika Mahafali hayo Mkuu wa Chuo hicho Rais Mstaafu wa Zanzibar wa awamu ya sita Mhe, Amani Abeid Karume amesema Elimu ni jambo muhimu kwa wanadamu na chuo hicho kitaendelea kutoa mchango wake kikamilifu kukuza Elimu hapa nchini.
