RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema uhusiano mzuri uliopo baina ya Zanzibar na India umenedelea kuimarika.Amesema, mbali na ushirikiano wakaribu uliopo baina ya Serikali za pande mbili hizo pia uhusiano kati ya Wahindi na Watanzania ni wa muda mrefu na diaspora wengi raia wa India wapo nchini kwa miaka mingi wakiwa na shughuli mbalimbali za jamii na uchumi.

Rais Dk. Mwinyi aliyasema hayo Ikulu, Zanzibar alipomkaribisha kwa mara ya kwanza Zanzibar, Waziri wa nchi na mambo ya Nje wa India, Mhe. Shri V. Muraeedharan.Rais Dk.Mwinyi alisema India imekua ikiiunga mkono Tanzania husuasa Zanzibar kwenye masuala mbalimbali ya maendeleo ikiwemo sekta ya maji na elimu kwa kutoa fursa nyingi za udhamini wa masomo nchini India kwa Watanzania wengi.

Aidha, Dk. Mwinyi alisema uamuzi wa India kuanzisha tawi la Chuo cha IIT madrsa kwa Zanzibar ni mafanikio makubwa ya ushirikiano uliopo baina ya India na Tanzania ikiwemo Zanzibar pia ni fursa azimu ya kuiweka Zanzibar kwenye ramani ya ulimwengu huku kukiwa na matumaini yakupokea wageni wengi kutoka nje ya Tanzania kuja kujiunga na chuo hicho Zanzibar

Pia, Rais Dk. Mwinyi alitaka ushirikianao baina ya chuo hicho na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuongeza vitivo vingi zaidi ya masimo chuoni hapo.Hata hivyo, Dk. Mwinyi aliishukuru seikali ya India kwa kuendelea kuziungamkono serikali za Tanzania kwenye sekta mbalimbali zamaendeleo.

Akizungumza kwenye hafla hiyo, Waziri Wanchi na Mambo ya Nje anaeshughulikia pia masuala ya Bunge nchini India, Shri V. Muraeedharan alisema licha ya mara yake ya kwanza kuzuru Tanzania lakini uhusiano baina ya India Zanzibar ulianza kabla ya Tanganyika na Zanzibar kuungana, historia iliyoziunganisha pande mbili hizo kiuchumi na jamii.

Akizungumzia uamuzi wa India kuanzisha tawi la chuo cha IIT Madrasa Zanzibar, Waziri Muraeedharan alisema ni njia moja ya kudumisha Dipomasia iliopo baina ya Tanzania hususan Zanzibar na India sambamba na kuzalisha viongozi wengi wenye fani na teknolojia ya hali ya juu kutoka kampasi ya Zanzibar.Katika ziara yake, Zanzibar Waziri Muraeedharan alipata fursa ya kutembelea chuo cha IIT Madrasa kilichopo Bweleo, Wilaya ya Magharibi ‘B’ pamoja na kuangalia eneo litakalijengwa chuo cha IIT Madrasa, Kampasi ya Zanzibar Fumba.

Hafla hiyo pia, ilihudhuriwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Lela Muhamed Mussa, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, Zanzibar, Mwanahamisi Ameir, Balozi wa India nchini Tanzania Mhe. Binaya Pradhan na Balozi Mdogo wa India aliepo Zanzibar, Dk. Kumar Praveen