Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt, Hussein Ali Mwinyi amewaapisha Wakuu wa Mikoa na Manaibu Makatibu wakuu alyowateuwa hivi Karibuni.Hafla hiyo ya Uapisho imefanyika leo tarehe 17 Disemba 2025 Ikulu ,Mkoa wa Mjini Magharibi.
Walioapishwa ni Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Nd Cassian Gallos Nyimbo na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Muhammed Ali Abdalla.
Manaibu Makatibu Wakuu walioapishwa ni Nd, Hawaah Ibrahim Mbaye Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasilino, Teknolojia ya Habari na Ubunifu , na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda Dkt, Said Seif Mzee.
