Media » News and Events

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi ameivunja Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Bima la Zanzibar (ZIC)

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi ameivunja Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Bima la Zanzibar(ZIC) kuanzia tarehe 18 Agosti, 2021 Na kumteuwa Bwana Ramadhan Mwalim Khamis kuwa Mwenyekiti mpya wa Bodi hiyo.

Uteuzi huo unaanzia tarehe 18 Agosti, 2021

Aidha, Mhe. Rais Dk. Mwinyi amemteuwa Mhe. Balozi Amina Salum Ali kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Takwimu Zanzibar kuanzia tarehe 16 Agosti, 2021.

Mhe. Rais Dk. Mwinyi pia amefanya uteuzi wa Mwenyekiti na Mkurugenzi wa Baraza la Taifa la Watu wenye Ulemavu kama ifuatavyo;

1) Bibi Salma Haji Saadat ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Watu wenye Ulemavu.


2) Bwana Ussy Khamis Debe ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Baraza la Taifa la Watu wenye Ulemavu.


Uteuzi huo umeanzia tarehe 18 Agosti, 2021.

Download File: