SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema daima inaungamkono jitihada za wadau wa mendendeleo nchini na kwamba inathamini michango na huduma wanazozitoa kwa Serikali na wananchi kwa ujumla.Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi aliyasema hayo Ikulu, Zanzibar alipozungumza na wajumbe wa bodi na watendaji kutoka benki ya CRDB waliofika kumkabidhi mfano wa Kadi ya benki ya Al barakaah ya CRDB.
Dk. Mwinyi aliipongeza benki hiyo kwa huduma wanazozitoa kwa wananchi wa Zanzibar na Watanzania kwa ujumla.Pia aliwasihi kudumisha ushirikiano wao baina ya sekta ya binafsi na taasisi za umma ili wapate mafanikio makubwa zaidi.Rais Dk. Mwinyi aliishukuru benki hiyo kwa heshima kubwa waliyompa kuwa mteja wao wa kunzwa kwa Zanzibar kupokea huduma za benki ya Al barakaah.
“Natoa shukurani zangu kwa heshima kubwa mliyonipa, hii ni shughuli ya kutoa kadi na ya kwanza mmenipa mimi” alishukuru Dk. Mwinyi.Aidha, Rais Dk. Mwinyi aliueleza uongozi wa benki hiyo mwamba Serikali inaungamkono jitiha na huduma wanazozitoa benki hiyo kwa Zanzibar. Pamoja na kuwapongeza kwa mafanikio makubwa waliyoyapata ndani ya kipindi kifupi tokea kuanzisha huduma za Al barakaah kwa visiwa vya Unguja na Pemba.
Akizungumza kwenye hafla hiyo, Mwenyekiti wa huduma za benki za Kiislam za Al barakaah za CRDB, Abdul Van Mohamed, alisema benki hiyo tokea imeanzisha huduma zinazofuata misingi ya Kiisslam (Al barkaah benki) wamepata mfanikio makubwa ndani ya kipindi cha miaka miwili.“Hadi sasa tumefanikiwa kupata wateja zaidi ya 70, 000 kwa Tanzania nzima, tumetoa mikopo inayofuata sharia za dini ya kiislam shilingi 87bil na tumefanikiwa kuhifadhi amana za wateja zinazosimamiwa kwa misingi sharia shilingi bilioni 95 kwa nchi nzima” alifafanua.
Alisema CRDB imetoa mchango mkubwa kwenye ujumuishi wa kifedha nchini pamoja na maendeleo ya kiuchumi kwa taifa na wananchi kwa ujumla nakuongeza kuwa tokea kuanzishwa kwa huduma hizo nchini kumekuwa na uhitaji mkubwa zimepokewa na wananchi kwa uitikio mkubwa.Van alieleza CRDB Al barakaah kwa Zanzibar imekua na mchango mkubwa kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Wananchi wake kwa kuwapa huduma nyingi ikwemo mikopo ya uchumi wa buluu, alisema zaidi ya bilioni 18 wamepewa wananchi wa Zanzibar kupitia dirisha la Al barakaah benki pia masoko zaidi ya bilioni 10 yametolewa kupitia dirisha hilo.
Aidha, alieleza benki hiyo ilifanikiwa kutoa mikopo inayofuata sharia kwa wafanya biashara na waajiriwa wa Zanzibar zaidi ya bilioni 10, amana za wateja zaidi ya bilioni 28 kwa zanzibar pekee, CRDB.Akizungumzia mfano wa kadi za “Al barakaah benki” Mkuu wa kitengo cha Al barakaah benki ya CRDB, Rashid Rashi alisema mwenekano wake zinaendana na matakwa na matarajio ya wateja wao kwa kujua pesa zao zipo mikono salama na uangalizi maalumu unaoendana na imaani na maadili ya sharia za wateja wao.
Alisema kadi hizo zimeunganishwa na mifumo ya kimataifa inampa uhuru mteja kufanya miamala sehemu yeyeote duniani za huduma za ATM , kwa upande wa Tanzania alieleza kadi hizo zinauwezo wa kutumika kwenye ATM zisizopungua 600, mawakala zaidi ya elfu 28 na matawi kwa Tanzania nzima zaidi ya 240.
Kwa upande wa Zanzibar alisema kuna matawi manne, wakala zaidi ya 240 na ATM 19 kwa Unguja na Pemba ambako huduma za Al barakaah benki zinapatikana.Aidha, kwa tawi la Wete, Pemba, Mkuu kuyo alieleza tokea lilipofunguliwa mwaka jana kutokana na maelekezo ya Rais Dk. Mwinyi, kwamba benki hiyo ifungue tawi Wete ili iendeleze uchumi wa wananchi wa eneo hilo na tokea ilipofunguliwa mwaka jana, tayari imefanikiwa kuwa na amana za wateja shilingi bilioni 3.3, mikopo zaidi ya bilioni 2.7 na wateja zaidi ya 2,200.
Alisema amanda zote zimewekwa upande wa Sharia benki kama mahitaji ya wateja wao yalivyo na kueleza kuwa imekua chachu kwa upande wa Pemba.Rais Dk. Mwinyi anakuwa mteja wa kwanza kwa Zanzibar kufungua hesabu ya benki ya Al barakaah ya CRDB pia ni wakwanza kupokea kadi ya ATM ili afurahie huduma hizo za benki hiyo.