Kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya Kifungu cha 54 cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 na Kifungu cha 11(1) cha Sheria ya Wakala wa Usajili wa Matukio ya Kijamii Zanzibar Namba 3 ya mwaka 2018,
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein amemteua BWANA IDRISSA SHAABAN ZAHARAN kuwa MKURUGENZI MTENDAJI WA WAKALA WA USAJILI WA MATUKIO YA KIJAMII ZANZIBAR katika Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalumza SMZ.
Bwana Idrissa Shaaban Zahran anachukua nafasi ya Dkt. Hussein Khamis Shaaban ambaye atapangiwa kazi nyengine.
Uteuzi huo unaanzia leo tarehe 03 Machi, 2020.