Mgombea wa Nafasi ya Rais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt, Hussein Ali Mwinyi amehitimisha Kqmpeni za Chama Cha Mapinduzi kwa Pemba na kuwasisitiza Wananchi kukichagua ili kiendelee kuleta Maendeleo na Kuzitunza Tunu za Taifa.Rais Dkt, Mwinyi ameyasema hayo leo tarehe 23 Oktoba 2025 katika Ufungaji wa Kampeni za Chama Cha Mapinduzi kwa Upande wa Pemba katika Uwanja wa Michezo wa Micheweni ,Mkoa wa Kusini Pemba.

Dk,Mwinyi amesema CCM ina kila sababu ya kuchaguliwa tena kutokana na kutekeleza kwa Mafanikio Ilani yake ya 2020-2025 na kuvuka malengo katika sekta mbalimbali za Maendeleo ikiwemo Miundombinu, Afya ,Elimu ,Kilimo na Uwezeshaji Wananchi kiuchumi.Rais Dkt, Mwinyi ameeleza kuwa Katika Awamu ijayo Serikali atakayoiongoza baada ya kupata ridhaa ya Wazanzibar inalenga kutekeleza mipango mikubwa ya Maendeleo kasi kubwa zaidi.

Ameyataja Maeneo ambayo Serikali inaenda kuyatekeleza kuwa ni pamoja na Ujenzi wa Viwanda maeneo ya Dunga zuze na Chamanangwe Pemba kwa dhamira ya kuzalisha ajira kwa Vijana na Uwezeshaji Wananchi kiuchumi kwa kuwapatia Mikopo isio na riba.Aidha ameahidi Ujenzi wa Miundombinu ya barabara za lami kwa Barabara zote za ndani za Wilaya na Mikoa yote Unguja na Pemba.

Akizungumzia sekta ya Elimu amesema Serikali itaendelea kujenga skuli nyingi zaidi ikiwemo 20 za ghorofa na Dakhalia na tayari Serikali imeshaingia Mkataba na Mkandarasi wa Mradi huo pamoja na kuahidi Upatikanaji wa Maji kwq kila shehia. Kuhusiana na Nishati ya Mafuta amesema Serikali ijayo itajenga Hifadhi ya Mafuta kwq ajili ya kuwa na Uhakika wa mafuta wakati wote.

Amewahakikishia Vijana kuwa Serikali inaenda kuzalisha ajira zaidi ya 350 na kutoa ajira katika sekta za Ualimu,  Afya , na Vikosi vya Ulinzi na Usalama pamoja na kuwawezesha Vijana ili kujiajiri Wenyewe.Akielezea kuhusu Mishahara amesema Seikali Ijayo itapandisha Mishahara kulingana na Ukuaji wa Uchumi na sio Vyenginevyo pamoja na kuendelea na Ujenzi wa Nyumba bora za Maendeleo za makaazi kwa kila Wilaya amba,o zitakuwq na bei .

Aki,ungumzia suala la Usafiri Baharini amesema Serikali italiwezesha Shirika la Meli ili liweze kununua Meli nyengene Mpya na kutoa huduma bora kwa Wananchi Unguja na Pemba.Akihitimisha kqmpeni za Chama Cha Mapinduzi kwa Upande wa Pemba Rais Dkt, Mwinyi amewaomba Wananchi kumchagua tena kwa kura nyingi aweze kuyatekeleza yote aliyoyaahidi katika Kampeni.