Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa  Dkt. Ali Mohamed Shein amefanya uteuzi wa viongozi katika Taasisi mbali mbali za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kama ifuatavyo:-


1. NAIBU KAMISHNA WA CHUO CHA MAFUNZO
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein amemteua SACP  Haji Hamdun Omar kuwa Naibu Kamishna  wa Chuo cha Mafunzo.

2. MKUU WA UTAWALA WA JESHI LA KUJENGA UCHUMI (JKU)
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein amemteua Luteni Kanali Mussa Mohammed Shaame kuwa Mkuu wa Utawala wa JKU.

3. MWENYEKITI WA BODI YA WAKURUGENZI YA SHIRIKA LA MELI NA UWAKALA
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein amemteua Bwana Abdi Omar Maalim kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Meli na Uwakala.

4. KATIBU TAWALA WA WILAYA MICHEWENI
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein amemteua Bwana Hassan Abdulla Rashid kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Micheweni.

5. KATIBU TAWALA WA WILAYA YA MKOANI
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein amemteua Bibi Miza Hassan Faki kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Mkoani.

6. NAIBU MKURUGENZI WA IDARA YA HABARI (MAELEZO) KATIKA WIZARA YA HABARI, UTALII, UTAMADUNI NA MICHEZO
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein amemteua Dkt Juma Mohamed Salum Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo) katika Wizara ya Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo.

7. NAIBU MKURUGENZI MKUU WA TAASISI YA UTAFITI WA MIFUGO
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein amemteua Kanali Ali Hassan kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo katika Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi.


Uteuzi wote huo umeanza tarehe 19 Juni 2017.