Dk.Shein amewasili Kisiwani Pemba kuhudhuria Sherehe za miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar Kitaifa
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mhe. Hemed Suleiman Abdallah, alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Karume Kisiwani Pemba,kwa ajili ya kuhudhuria Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar zinazotarajiwa kufanyika tarehe 12/1/2019, katika Uwanja wa Gombani Pemba.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Viongozi wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama Kisiwani Pemba, baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Karume Mjini Chake chake Kisiwani Pemba.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mhe. Hemed Suleiman Abdallah, baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Karume Chake chake Kisiwani Pemba, akielekea katika chumba cha VIP.
Dk.Shein ametunuku Nishani ya Mapinduzi,Utumishi uliotukuka na Nishani ya Ushujaa.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa ameshimama wakati ukipigwa wimbo la Taifa baada ya kuwasili katika viwanja vya Ikulu Zanzibar, kwa ajili ya Kutunuku Nishani za Mapinduzi kwa Viongozi na Wananchi kuadhimisha Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Mkuu wa Brigedi ya Nyuki Zanzibar Brigedia Jenerali Fadhil Nondo, baada ya kumaliza hafla ya Kutunuku Nishani za Mapinduzi na Uongozi Uliotukuka, kushoto Katika Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiteta na Rais Mstaaf wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Awamu ya Pili Mzee. Ali Hassan Mwinyi, wakiwa katika viwanja vya Ikulu Zanzibar, wakati wa hafla ya kutunuku kwa Nishani za Mapinduzi na Uongozi Uliotukuka.
RAIS Mstaaf wa Tanzania Awamu ya Pili Mhe. Ali Hassan Mwinyi , akisalimiana na Mke wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume, Mama Fatma Karume, alipowasili katika viwanja vya Ikulu mjini Zanzibar, kuhudhuria hafla ya kutunukiwa Nishani Viongozi na Wananchi.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akisoma kitabu cha Orodha ya Viongozi na Wananchi wanaotunukiwa Nishani katika viwanja vya Ikulu Zanzibar.
BAADHI ya Viongozi wa Serikali wakiwa wamesimama wakati ukipigwa Wimbo wa Taifa katika viwanja vya Ikulu Zanzibar,wa kwanza Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja. Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud,Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu, Rais Mstaaf wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi, Mama Fatma Karume na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar. Mhe Zuberi Ali Maulid.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akimtunuku Nishani ya Mapinduzi kwa Viongozi Mhe. Omar Ramadhan Mapuri, hafla hiyo ya kutunuku Nishani ilifanyika katika viwanja vya Ikulu Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akimtunuku Nishani ya Ushujaa ya kujitolea kupiga mbizi katika pango la maji dimani kuchukua sampu ya mchanga ili kuweza kupata wingi wa maji Ndg. Ali Ameir Mwalim, hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Ikulu Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akimtunuku Nishaji ya Utumishi Uliotukuka Mwakilishi wa Marehemu Mussa Haji Foum, alikuwa Mwandishi wa Habari wa Vyombo vya Serikali vya Redio. akipokea kwa niaba ya Familia Mtoto wa Marehemu Bi.Inat Mussa Haji, hafla hiyo imefanyika katika Viwanja vya Ikulu mjini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akimtunuku Nishani ya Ushujaa Mwananchi wa Mkoa wa Kusini Unguja Ndg. Muhammad Haji Muhammad, kwa ujasiri aliouonesha kumuokoa mwananchi aliyeingia katika kisiwa na kumuokoa akiwa hai.hafla hiyo ya kutunuku Nishani za Mapinduzi ilifanyika katika viwanja vya Ikulu mjini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akimtunuku Nishaji ya Vikundi vya Uhamasishaji wa Bendi ya Safari Trippers ya Marehemu Marijan Rajab, akipokea Mwakilishi wa Familia Ndg Ismail Issa Michuzi, alikuwa Katibu na Mpiga Trumpet Dar International, hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Ikulu mjini Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa katika picha ya pamoja na Wananchi waliotunukiwa Nishani ya Mapinduzi na Uongozi Uliotukuku, baada ya hafla ya kukabidhiwa Nishani hizo katika viwanja vya Ikulu Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi na Wawakilishi wa Familia za Marehemu waliowakilisha katika kupokea Nishani kwa niaba ya familia.
Baadhi ya Viongozi Wastaaf na Wawakilishi wa Marehemu wakiwa katika viwanja vya Ikulu Zanzibar wakisubiri kutunukia Nishani za Mapinduzi na Utumishi Uliotukuka
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi na Wawakilishi wa Familia za Marehemu waliowakilisha katika kupokea Nishani kwa niaba ya familia.
BAADHI ya Wananchi na Viongozi Wastaaf waliotunikiwa Nishani ya Mapinduzi na UYongozi Uliotukuka wakitoka katika viwanja vya Ikulu Zanzibar baada ya kumalizika kwa hafla hiyo ya kutunukiwa Nishani na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein.
BENDI ya Brassband ya Jeshi la Polisi Zanzibar ikitowa burudani wakati wa hafla ya Utuaji wa Nishaji ya Mapinduzi na Uongozi Uliotukuka,katika viwanja vya Ikulu Zanzibar.
Rais wa zanzibar Dk.Shein amefungu Skuli ya Sekondari na Msingi Bwefum.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akikata utepe kuashiria kuifungua Skuli ya Sekondari na Msingi ya Bwefum Wilaya ya Magharibi B Unguja kulia Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud na kushoto Waziri wa Elimu na Mafunzio ya Amali Zanzibar Mhe. Rizi Pembe Juma,Skuli hiyo imejengwa na Kampuni ya Union Property Developers Ltd, ikiwa ni shamra shamra za kuadhimisha miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Riziki Pembe Juma, wakati Rais wa Zanzibar akitembelea moja ya Madarasa hayo alipotembelea baada ya kuifungua rasmin Skuli hiyo, ikiwa ni shamrashamra za miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akihutubia wakati wa ufunguzi wa Skuli ya Kisasa ya Sekondari na Msingi ya Bwefum, Wilaya ya Magharibi B Unguja, ikiwa ni shamrashamra za kuadhimisha miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
WANAFUNZI wa Skuli ya Msingi Bwefum Wilaya ya Magharibi B Unguja Masoud Mussa, Naifat Makame na Suleiman Sapu, wakiimba wimbo wa "Sisi Sote Tumegomboka " wakati wa hafla ya Ufunguzi wa Skuli yao,iliofunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe,. Dk. Ali Mohamed Shein, Skuli hiyo imejengwa na Kampuni ya Union Property Developers Ltd
WAZIRI wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Riziki Pembe Juma akizungumza kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmin Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, kuwahutubia Wananchi na kuifungua rasmin Skuli hiyo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein,akimsikiliza Mkandarasi aliyejenga Majengo ya Skuli hiyo kutoka Kampuni ya Ujenzi ya Quality Bulding Contractors Ltd. Mkurugenzi ,Mtendaji Ndg. Shaib Said Ali, akitowa maelezo ya Majenzo ya Skuli hiyo yaliotengenezwa na Mwanafunzi wa Skuli ya Sekondari ya Bwefum Kidatu chaTatu Khamis Masoud
Dk.Shein afungua jengo jipya la Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiondoa kipazia kuashiria kuweka Jiwe la Msingi la Jengo Jipya la Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, pamoja na Uzinduzi wa Maabara ya Vinasaba.(DNA),hafla hiyo imefanyika maruhubi Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiondoa kipazia kuashiria kuweka Jiwe la Msingi la Jengo Jipya la Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, pamoja na Uzinduzi wa Maabara ya Vinasaba.(DNA),hafla hiyo imefanyika maruhubi Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.mDk. Ali Mohamed Shein, akisoma jiwe la msingi baada ya kulizindua jengo jipya la Mkemia Mkuu wa Serikala Maruhubi Zanzibar, kushoto Kaimu Waziri wa Afya Zanzibar, Waziri wa Kilimo,Maliasili Mifugo na Uvuvi Mhe Rashid Ali Juma.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akikata utepe kuashiria kulifungua Jengo Jipya la Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali Maruhubi Zanzibar, kushoto Kaimu Waziri wa Afya Zanzibar, Waziri wa Kilimo Maliasili Mifugo na Uvuvi Mhe. Rashid Ali Juma.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Mchunguzi wa Maabara ya Vinasaba (DNA) (Genitic Analyzer) Bi. Saide Abdalla Mbarak,akitowa maelezo ya matumizi ya mashine hiyo wakati wa ufunguzi wa Maabara ya Vinasaba (DNA) wakati wa hafla ya uzinduzi wa Jengo la Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali Maruhubi Zanzibar, ikiwa ni shamrashamra za kuadhimisha Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Mkemia Mkuu wa Serikali Dkt. Slim Rashid Juma, akitowa maelezo ya picha ya jengo hilo jipya la Mkemia Mkuu baada ya kulifungua rasmin, ikiwa ni shamrashamra za kuadhimisha miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Mchunguzi Maabara ya (DNA ) Vinasaba,(Genetic Analyzer) Bi. Saide Abdalla Mbarak, akitowa maelezo ya moja ya Vifaa vya DNA wakati wa uzinduzi huo wa Maabara ya Vinasaba uliofanyika katika jengo jipya la Mkemia Mkuu Maruhubi Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiongozana na Kaimu Waziri wa Afya na Waziri wa Kilimo,Maliasili Mifugo na Uvuvi Mhe. Rashid Ali Juma wakiongea wakati wakielekea katika eneo maalum kwa ajili ya kuzungumza na Wananchi na Wafanyakazi wa Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali baada ya Uzinduzi wa Jengo Jipya na Maabara ya Vinasaba (DNA) ikiwa ni shamrashamra za kuadhimisha miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
WAFANYAKAZI wa Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali wakishangilia wakati wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akihutubia katika hafla ya Uzinduzi wa Jengo Jipya la Mkemia Mkuu wa Serikali Maruhubi.
Mhe: Dk.Shein aweka jiwe la msingi jengo la Zura Maisara Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiondoa kipazia kuashiria kuweka Jiwe la Msingi la Jengo ZURA Maisara Zanzibar, ikiwa ni shamrashamra za Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar, kulia Waziri wa Ardhi, Nyumba,Maji na Nishati Zanzibar Mhe.Salama Aboub Talib, akishuhudia uwekaji wa jiwe la msingi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akisoma Jiwe la Msingi la Jengo la ZURA Maisara, baada ya kuweka jiwe hilo, ikiwa ni shamrashamra za Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar, hafla hiyo imefanyika, 6-1-2019, katika eneo hilo la Maisara.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akitembelea jengo hilo la ZURA, baada ya hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi la jengo hilo, akipata kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa ZURA Ndg.Haji Kali Haji, kulia na kushoto Waziri wa Ardhi,Nyumba,Maji na Nishati Zanzibar Mhe. Salama Aboud Talib, akitembelea jengo hilo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa ZURA Ndg. Haji Kali Haji, akitowa maelezo ya michoro ya picha ya jengo hilo haiko pichani wakati wa hafla ya uzinduzi wa uwekaji wa Jiwe la Msingi, ikiwa ni shamrashamara za kuadhimisha Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar
Jengo jipya la ZURA liliopo Maisara Zanzibar litakuwa na gorofa saba litakapomalizika ujenzi wake unaojengwa na Kampuni ya Kichina ya Hainan International Ltd.
Wafanyakazi wa Kampuni ya Kichina ya Hainan International Ltd,wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, wakati akihutubia katika hafla hiyo ya uwekaji wa jiwe la msingi la jengo la ZURA Maisara Zanzibar ikiwa ni shamrashamra za Miaka 55 Mapinduzi ya Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa na Viongozi wa Serikali na Wajenzi wa jengo la ZURA.katika picha ya pamoja baada ya uwekaji wa jiwe la msingi.
Wafanyakazi wa ZURA wakifuatilia hutuba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akihutubia wakati wa hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi la jengo jipya la Wizara ya Ardhi,Nyumba,Maji na Nishati Zanzibar
Waziri wa Ardhi Nyumba Maji na Nishati Zanzibar Mhe. Salama Aboud Talib akihutubia wakati wa hafla hiyo ya uwekaji wa jiwe la msingi wa Jengo la ZURA Maisara Zanzibar.
Wafanyakazi wa ZURA wakifuatilia hutuba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akihutubia wakati wa hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi la jengo jipya la Wizara ya Ardhi, Nyumba,Maji na Nishati Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akihutubia wakati wa hafla ya Uwekaji wa Jiwe la Msingi la Jengo la ZURA Maisara Zanzibar ikiwa ni shamrashamra za kuadhimisha Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.