State House Blog

Ufunguzi wa Msikiti wa Ijumaa Chuini Zanzibar.

 • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi (wa nne kulia) akijumuika na Viongozi na Waumini wa Dini ya Kiislamu katika sala ya Ijuma mara baada ya Kufungua Masjid Muhammed Bin Ahmed Al Jofair uliopo Chuini Wilaya ya Magharibi A Unguja, uliojengwa kupitia Wafadhili na Waislamu mbali mbali, ambapo sala ilioongozwa na Sheikh Rashid Salim (mbele).
 • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi (kushoto) akitoa nasaha zake kwa waumini wa dini ya Kiislamu baada ya ufunguzi wa Masjid Muhammed Bin Ahmed Al Jofair, Chuini Wilaya ya Magharibi A Unguja, uliojengwa kupitia Wafadhili na michango ya Waislamu mbali mbali.
 • Waumini wa Dini ya Kiislamu wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) alipokuwa akitoa nasaha zake kwa waumini hao baada ya sala ya Ijumaa na ufunguzi wa Masjid Muhammed Bin Ahmed Al Jofair, Chuini Wilaya ya Magharibi A Unguja, uliojengwa kupitia Wafadhili na michango ya Waislamu mbali mbali.
 • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Viongozi wakati alipowasili leo katika Ufunguzi wa Masjid Muhammed Bin Ahmed Al Jofair uliopo Chuini Wilaya ya Magharibi A Unguja.
 • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi (kulia) akifungua pazia kuashiria Ufunguzi wa Masjid Muhammed Bin Ahmed Al Jofair uliopo Chuini Wilaya ya Magharibi A Unguja, uliojengwa kupitia Wafadhili na Waislamu mbali mbali.
 • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi (katikati) akikata utepe kama ishara ya ufunguzi wa Masjid Muhammed Bin Ahmed Al Jofair uliopo Chuini Wilaya ya Magharibi A Unguja, uliojengwa kupitia Wafadhili na Waislamu mbali mbali.

Mjadala kukuza uwekezaji wa Makampuni ya Ulaya Nchini

 • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Balozi wa Jumuiya ya Umoja wa Ulaya Nchini Tanzania Bw.Manfredo Fanti (kushoto) wakati alipowasili katika Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Zanzibar katika mjadala wa Kukuza uwekezaji wa Makampuni ya Ulaya nchini Zanzibar.
 • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi (kulia) akiteta na Balozi wa Jumuiya ya Umoja wa Ulaya Nchini Tanzania Bw.Manfredo Fanti kabla ya mjadala wa Kukuza uwekezaji wa Makampuni ya Ulaya nchini Zanzibar uliofanyika leo katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Zanzibar.
 • Wadau na waalikwa mbali mbali wakiwa katika mjadala wa Kukuza uwekezaji wa Makampuni ya Ulaya nchini Zanzibar uliofanyika leo ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Zanzibar.
 • Wadau na waalikwa mbali mbali wakiwa katika mjadala wa Kukuza uwekezaji wa Makampuni ya Ulaya nchini Zanzibar uliofanyika leo ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Zanzibar.
 • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi (katikati) na Balozi wa Netherland Nchini Tanzania Mhe.Wiebe de Boer wakishuhudia Utiaji saini wa Ushirikiano baina ya Serikali ya Mapinduzi na Jumuiya ya Ulaya katika mjadala wa Kukuza uwekezaji wa Makampuni ya Ulaya Nchini Zanzibar uliofanyika leo ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Zanzibar (kulia) Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Uwekezaji na Vitega Uchumi ZIPA Nd,Sharif Ali Sharif na (kushoto)Mkurugenzi Mtendaji anaeiwakilisha Jumuiya hiyo Cikay Richards.
 • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi (katikati) akifuatana na Balozi wa Jumuiya ya Umoja wa Ulaya Nchini Tanzania Bw.Manfredo Fanti (wa pili kulia) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Kazi,Uchumi na Uwekezaji Mhe.Mudrik Ramadhan Soraga na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Idrissa Mustafa Kitwana (kushoto) kabla ya kuingia katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Zanzibar katika mjadala wa Kukuza uwekezaji wa Makampuni ya Ulaya nchini Zanzibar uliofanyika leo .
 • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi (katikati) pamoja na wadau mbali mbali na Balozi wa Jumuiya ya Umoja wa Ulaya Nchini Tanzania Bw.Manfredo Fanti ( kushoto) na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Kazi,Uchumi na Uwekezaji Mhe.Mudrik Ramadhan Soraga (wa tatu kulia) wakisimama wakati Wimbo wa Taifa ukipigwa katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Zanzibar katika hafla ya mjadala wa Kukuza uwekezaji wa Makampuni ya Ulaya nchini Zanzibar uliofanyika leo
 • Wadau na waalikwa mbali mbali wakiwa katika mjadala wa Kukuza uwekezaji wa Makampuni ya Ulaya nchini Zanzibar uliofanyika leo ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Zanzibar.
 • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi (katikati) pamoja na Viongozi mbali mbali, Balozi wa Netherland Nchini Mhe.Wiebe de Boer (kushoto)Balozi wa Jumuiya ya Umoja wa Ulaya Nchini Tanzania Bw.Manfredo Fanti ( wa pili kushoto) Balozi wa Netherland Nchini Tanzania Mhe.Wiebe de Boer na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Kazi,Uchumi na Uwekezaji Mhe.Mudrik Ramadhan Soraga (wa tatu kulia) wakifuatilia kwa makini mjadala wa Kukuza uwekezaji wa Makampuni ya Ulaya nchini Zanzibar uliofanyika leo ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Zanzibar.
 • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi alipokuwa akitoa hutuba yake katika mjadala wa Kukuza uwekezaji wa Makampuni ya Ulaya nchini Zanzibar uliofanyika leo katika Ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Zanzibar ambapo wadau mbali mbali wamehudhuria katika mjadala huo

Rais wa Zanzibar Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amezungumza na Mkuu wa Idara ya Afrika Mfuko wa “Global Fund” Bw. Linden Morrison Ikulu Zanzibar.

 • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Mkuu wa Idara ya Afrika Mfuko wa “Global Fund” kutoka Geneva Bw. Linden Morrison, alipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu leo 10-6-2022, akiongozana na ujumbe wake
 • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiagana na Mkuu wa Idara ya Afrika Mfuko wa “Global Fund” kutoka Geneva Bw. Linden Morrison, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar leo 10-6-2022, akiwa na ujumbe wake.
 • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Mkuu wa Idara ya Afrika Mfuko wa “Global Fund” kutoka Geneva Bw.Linden Morrison, alipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo akiwa na ujumbe wake Dr.Sarah Asiimwe na Dr. Patrick Githendu, mazungumzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu leo 10-6-2022.

Rais Dk.Hussein Ali Mwinyi ameshiriki swala ya Ijumaa katika Mskiti wa Masijd Sunna uliopo Kikwajuni Zanzibar.

 • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi (wa pili kulia) akiitikia dua iliyoombwa na Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Mahmoud Mussa Wadi (wa pili kushoto) leo mara baada ya swala ya Ijumaa liyoswaliwa katika Masjid Sunna Kiwajuni Jijini Zanzibar Mkoa wa Mjini Magharibi.
 • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi (kushoto) akisalimiana na Sheikh Kassim Haidar Jabbir Alfarsiy leo mara baada ya swala ya Ijumaa katika Masjid Sunna Kiwajuni Jijini Zanzibar Mkoa wa Mjini Magharibi.
 • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi leo ameshiriki swala ya Ijumaa na Waumini mbali mbali katika Masjid Sunna Kiwajuni Jijini Zanzibar Mkoa wa Mjini Magharibi.
 • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi leo ameshiriki swala ya Ijumaa na Waumini mbali mbali katika Masjid Sunna Kiwajuni Jijini Zanzibar Mkoa wa Mjini Magharibi.
 • Waumini wa Dini ya Kiislamu katika Masjid Sunna Kikwajuni Jijini Zanzibar wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) alipotoa nassaha zake leo mara baada ya swala ya Ijumaa katika Masjid Sunna Kiwajuni Jijini Zanzibar Mkoa wa Mjini Magharibi.

Rais wa Zanzibar Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amekabidhiwa msaada wa Vifaa Tiba na dawa kutoka kwa Madaktari Bingwa wa Jamhuri ya watu wa China wanaotoa huduna za Afya katika Hospitali za Unguja na Pemba

 • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Kiongozi wa Madaktari Bingwa kutoka China Dr.Qu Lishuai wakati akikabidhi Vifaa Tiba kwa ajili ya matumizi ya Hospitali ya Rufaa ya Mnazi Mmoja Unguja,Kivunge Mkoa wa Kaskazini Unguja, Chake chake Pemba na Hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani Pemba, hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar leo 7-6-2022. (Kulia kwa Dr Qu ) Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Nassor Ahmed Mazrui.
 • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Madaktari Bingwa wa Kichina wanaotoa huduma za Afya katika Hospitali za Unguja na Pemba, walipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo na kukabidhi Vifaa Tiba na Dawa mbalimbali kwa ajili ya Hospitli ya Kuu ya Rufaa ya Mnazi Mmoja Zanzibar,Kivunge Mkoa wa Kaskazini Unguja,Chake chake Pemba na Hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani Pemba, hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar
 • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Madaktari Bingwa wa Kichina wanaotoa huduma za Afya katika Hospitali za Unguja na Pemba, walipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo na kukabidhi Vifaa Tiba na Dawa mbalimbali kwa ajili ya Hospitli ya Kuu ya Rufaa ya Mnazi Mmoja Zanzibar,Kivunge Mkoa wa Kaskazini Unguja, Chake chake Pemba na Hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani Pemba, hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar.
 • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Madaktari Bingwa wa Kichina wanaotoa huduma za Afya katika Hospitali za Unguja na Pemba, walipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo na kukabidhi Vifaa Tiba na Dawa mbalimbali kwa ajili ya Hospitli ya Kuu ya Rufaa ya Mnazi Mmoja Zanzibar,Kivunge Mkoa wa Kaskazini Unguja, Chake chake Pemba na Hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani Pemba, hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar.
 • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Madaktari Bingwa kutoka Kichina wakiongozwa na Dr. Qu Lishuai (kulia kwa Rais) alipowasili katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar, walipofika kwa ajili ya mazungumzo na kukabidhi Vifaa Tiba kwa ajili ya Hospitali za Mnazi Mmoja, Kivunge,Chakechake Pemba na Hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani Pemba.
 • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Kiongozi wa Madaktari Bingwa kutoka Kichina Dr. Qu Lishuai akizungumza na kuwatambulisha Madaktari Bingwa wanaotowa huduma za afya katika Hospitali za Unguja na Pemba, wakati wa hafla ya kukabidhi Vifaa Tiba , hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar leo 7-6-2022.