State House Blog

Rais wa Zanzibar Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi amejumuika katika Futari maalum aliyowaandalia wananchi wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.

  • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na kuwaaga Wananchi baada ya kumalizika kwa hafla ya futari maalum aliyowaandalia katika ukumbi wa jengo la Michezani Mall Jijini Zanzibar.
  • WANANCHI wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja wakiitikia dua ikisomwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Saleh Omar Kabi (hayupo pichani)baada ya kumalizika kwa hafla ya futari maalum ilioandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi kwa Wananchi wa Mkoa huo, iliofanyika katika ukumbi wa jengo la Michezani Mall Jijini Zanzibar
  • MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akiitikia dua ikisomwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Saleh Omar Kabi. (hayupo pichani)baada ya kumalizika kwa hafla ya futari maalum iliyoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi.(hayupo pichani) katika ukumbi wa jengo la Michezani Mall, kwa Wananchi wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja na (kushoto kwake) Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said na (kulia kwake) Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais.Mhe.Dkt. Saada Mkuya Salum na Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Mhe.Lela Mohammed Mussa.wakiitikia dua.
  • WANANCHI wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja wakiitikia dua ikisomwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Saleh Omar Kabi (hayupo pichani)baada ya kumalizika kwa hafla ya futari maalum ilioandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi kwa Wananchi wa Mkoa huo, iliofanyika katika ukumbi wa jengo la Michezani Mall Jijini Zanzibar.
  • BAADHI ya Viongozi wa Vyama vya Siasa na Wananchi wakiitikia dua ikisomwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Saleh Omar Kabi (hayupo pichani) baada ya kumalizika kwa hafla ya futari maalum ilioandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi.(hayupo pichani) iliofanyika katika ukumbi wa jengo la Michezani Mall Jijini Zanzibar.