State House Blog

Rais wa Zanzibar Mhe. Dk.Hussein Mwinyi amezindua Maadhimisho ya Miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar katika Viwanja vya Nyamanzi Zanzibar.

  • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi, akimsikiliza Mkurugenzi wa (BOT) Tawi la Zanzibar Camillus Kombe,wakati akitembelea banda la maonesho la (BOT) katika viwanja vya Maonesho Nyamanzi Dimani Ndambani Wilaya ya Magharibi “B”, wakati wa Uzinduzi wa Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, (kushoto kwa Rais) Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla na (kulia kwa Rais) Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe.Dkt. Selemani Jafo na Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe.Zuberi Ali Maulid.14-4-2024
  • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi, akimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar Fatma Mabrouk Khamis ,wakati akitembelea banda la maonesho la Wizara hiyo katika viwanja vya Maonesho Nyamanzi Dimani Ndambani Wilaya ya Magharibi “B”, Unguja, wakati wa Uzinduzi wa Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, (kushoto kwa Rais) Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Mhe.Ayoub Mohammed Mahmoud.14-4-2024
  • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi na (kulia kwa Rais) Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla,wakimsikiliza Katibu Msaidizi wa Tume ya Pamoja ya Fedha (JFC) Jonas Nduttu, wakati akitembelea banda la maoneshe la (JFC) wakati wa Uzinduzi wa Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, yanayofanyika katika viwanja vya maonesho vya Nyamanzi Dimani Ndambani Wilaya ya Magharibi “B” Unguja leo 14-4-2024
  • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Viongozi mbalimbali wa Serikali alipowasili katika viwanja vya Nyamazi Dimani Ndambani Wilaya ya Magharibi “B” Unguja, kwa ajili ya Uzinduzi Rasmin wa Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, uliofanyika leo 14-4-2024 katika viwanja hivyo
  • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud, wakimsikiliza Afisa Masoko na Uhusiano wa Mfuko wa Huduma za Afya Zanzibar (ZHSF) Asha Kassim Biwii,wakati akitembelea banda la maoneshe la (ZHSF) wakati wa Uzinduzi wa Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, yanayofanyika katika viwanja vya maonesho vya Nyamanzi Dimani Ndambani Wilaya ya Magharibi “B” Unguja leo 14-4-2024
  • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk .Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi , wakimsikiliza Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Cyprian Luhemeja, wakati akitembelea banda la maoneshe la Wizara ya Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, wakati wa Uzinduzi wa Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, yanayofanyika katika viwanja vya maonesho vya Nyamanzi Dimani Ndambani Wilaya ya Magharibi “B” Unguja leo 14-4-2024
  • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akikabidhiwa zawadi maalum na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe.Dkt. Selemani Jafo, baada ya kutembelea baanda la maonesho la Ofisi hiyo wakati wa uzinduzi wa Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 60 ya Muungano wa Tanganika na Zanzibar, yanayofanyika katika viwanja vya Maonesho vya Nyamazi Dimani Ndambani Wilaya ya Magharibi “B” Unguja leo 14-4-2024