RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, amerejea nchini leo akitokea Uingereza.
Katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume viongozi mbali mbali wa Serikali, vyama vya siasa pamoja na wakuu wa vikosi vya ulinzi na usalama wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakiongozwa na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd walimpokea Rais Dk. Shein.
Dk. Shein katika safari hiyo, alifuatana na Mkewe Mama Mwanamwema Shein pamoja na Watendaji wengine wa Serikali.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama Zanzibar, alipowasili katika Uwanja wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar akitokea Nchini Uingereza, alipokuwa na
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein na Mkewe Mama Mwanamwema Shein,, akisalimiana na Wananchi waliofika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar kumpokea akitokea Nchini Uingereza kwa ziara Ma