Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amejumuika na viongozi wa dini na masheikh waliofika Ikulu leo, tarehe 21 Machi 2026, mara baada ya Sala ya Eid al-Fitr. Wakati huohuo,

Rais Dkt.Mwinyi ametoa Mkono wa Eid kwa mamia ya watoto na wananchi, wakiwemo wajane na wenye mahitaji maalum waliofika Ikulu. Aidha, Alhaj Dkt. Mwinyi amewatakia heri na baraka katika kusherehekea Sikukuu ya Idd el-Fitr.

Rais Dkt. Mwinyi ameendelea na utaratibu wake wa kudumu wa kutoa Mkono wa Eid kwa watu wa makundi maalum pamoja na watoto wakati wa Sikukuu hiyo.

Kabla ya Kutoa Mkono wa Eid kwa mamia ya watoto na wananchi waliofika hapo Ikulu Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amejumuika na waumini wa dini ya Kiislamu katika ibada ya Sala ya Eid al-Fitr iliyosaliwa leo, tarehe 21 Machi 2026, katika Msikiti wa Jamiu Zanjibar, Kiembe Samaki, Mkoa wa Mjini Magharibi.

Waumini wa dini ya Kiislamu wanasherehekea Sikukuu ya Eid al-Fitr baada ya kukamilika kwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Ibada hiyo imehudhuriwa na viongozi wa Serikali, viongozi wa dini pamoja na waumini mbalimbali wa dini ya Kiislamu.