RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amefanya uteuzi wa viongozi katika taasisi mbalimbali za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kama ifutavyo:-.
1.OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA SERIKALI ZA MITAA NA IDARA MAALUMU ZA SMZ.
I. Mkuu wa Wilaya ya wete – Kapteni Khatib Khamis Mwadini.
II. Mkuu wa Wilaya ya Magharibi A – Bwana Abeid Juma Ali.
III. Katibu Tawala wa Mkoa wa Mjini/ Magharibi – Bwana Saleh Mohamed Juma.
IV. Katibu Tawala wa Wilaya Magharibi A – Said Haji Mrisho.
V. Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Dkt.Haji Salim Khamis.
2.WIZARA YA BIASHARA NA VIWANDA
I. Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara na Viwanda – Juma Hassan Reli
II. Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Viwanda – Abdulla Rashid Abdulla
III. Ofisa Mdhamini wa Wizara ya Biashara na Viwanda Pemba Bwana Ali Suleiman Abeid.
3.TUME YA MIPANGO
i. Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango – Bwana Mwita Mgeni Mwita
ii. Kamishna wa Idara ya Ukuzaji wa Uchumi na Mashirikiano baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi – Dkt.Rahma Salim Mahfoudh.
iii. Mkurugenzi wa Idara ya Uendeshaji na Utumishi katika Tume ya Mipango – Bibi Maryam Nassor Uki.
4.WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI
i. Mwenyekiti wa Bodi ya Huduma za Maktaba – Bwana Yahya Idris Abdulwakil
ii. Mwenyekiti wa Bodi ya Mkaguzi Mkuu wa Elimu – Dkt.Ali Ussi Makame
5. WIZARA YA HABARI,UTALII NA MAMBO YA KALE
i. Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji la Zanzibar (ZBC) – Bwana Chande Omar Omar.
ii. Mkuu wa Chuo cha Uandishi wa Habari Zanzibar – Bibi Imane Osmond Duwe
Uteuzi huo umeanza leo tarehe 11 Juni 2019.