Kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya Kifungu cha 61(2) cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein amemteua
KAMANDA MOHAMED MUSSA SEIF (Mkobani) kuwa MKUU WA WILAYA YA WETE katika Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ. Kabla ya Uteuzi huo, Kamanda Mohamed Mussa Seif alikuwa Mkuu wa Kamandi ya KMKM Pemba.
Kamanda Mohamed Mussa Seif anachukua nafasi ya Kapteni Khatib Khamis Mwadini ambaye uteuzi wake umetenguliwa.
Uteuzihuounaanzialeotarehe 11 Juni, 2020.