Media » News and Events

Dk. Hussein Ali Mwinyi akiambatana na Mama Mariam Mwinyi pamoja na ujumbe wake amewasili Havana nchini Cuba

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi akiambatana na Mama Mariam Mwinyi pamoja na ujumbe wake amewasili Havana,nchini Cuba kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa nchi na Serikali wa kundi la 77 na China (G77+China)

Mkutano huo unatarajiwa kufunguliwa tarehe 15 Septemba ambapo Rais Dk. Mwinyi atamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.Katika uwanja wa ndege wa Jose Marti Rais Dk. Mwinyi alipokelewa na Balozi wa Tanzania Mhe.Balozi Humphrey H.Polepole na maafisa wengine wa ubalozi wa Tanzania Havana, Cuba.

Baadae Rais Dk. Mwinyi atafungua rasmi ubalozi wa Tanzania nchini humo.