RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi   Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema ameridhishwa na hatua zilizofikiwa za ujenzi katika Hospitali mpya ya Mkoa wa Mjini Magharibi, inayoendelea kujengwa katika eneo la Lumumba.Dk. Mwinyi amesema hayo leo katika ziara fupi alipotembelea Hospitali hiyo ili kuangalia maendeleo ya ujenzi wake.

Akizungumza na Viongozi, watendaji na wananchi walioshiriki katika ziara hiyo Dk. Mwinyi alisema amefurahishwa na kasi ya Mkandarasi anaendeleza mradi huo, ambapo hadi sasa hatua za ujenzi zimefikia asilimia 69 ya kazi yote.

Alisema kuna kila sababu ya kujivunia kwa uwepo wa Hospitali hiyo ambayo ni ya aina yake hapa Zanzibar.

Alisema Serikali ina matarajio makubwa kuwa Hospitali hiyo itakamilika ujenzi wake na kuanza kutumika ifikapo mwezi Aprili 2023 , na kuwa Hospitali mbadala katika kuendeleza tiba na kupisha ukarabati mkubwa unaotarajiwa kufanyika katika Hospitali ya Rufaa ya Mnazi Mmoja.

Aidha , alibainisha azma ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya kuhakikisha kila Mkoa hapa nchini unakuwa na Hospitali ya aina hiyo.

Wakati huo huo,  Dk. Mwinyi aliwatoa khofu wajasiriamali wanaojihusisha na kazi za kutengeneza vyombo vya moto ambao wamelazimika kusimamisha shughuli zao na kuhama eneo hilo ili kupisha ujenzi wa Hospitali hiyo.
Aliwathibitishia Wajasiriamali hao kuwa tathmini kwa ajili ya malipo yao tayari imefanyika na wanatarajiwa kulipwa katika kipindi kifupi kijacho.

Aidha, aliwawahikishia kuwekewa miundombinu muhimu katika sehemu yao mpya kazi .

Mapema, Waziri wa Afya Nassor Ahmed Mazrui alielezea maendeleo ya Kazi za ujenzi wa Hospitali hiyo na kusema kabla Hospitali hiyo ilitarajiwa kukamilika ujenzi wake mnamo mwezi Januari 2023 , lakini kutokana na changamoto ya kuibuka kwa Ugonjwa wa Covid – 19, baadhi ya vifaa vilivyotarajiwa kutumika vilichelewa kufika nchini. Hata hivyo akabainisha kuwa tayari mahitaji mengi ya vifaa yameshakamilika